Wananchi wa Kata ya Sandali Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam wameilalamikia Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia TAZARA kwa kubadilisha Sheria ya Mwaka 1975 ambayo ilikuwa inawataka Wananchi wasijenge nyumba za makazi ndani ya Mita 30 kutoka eneo la Reli Wananchi hao wamesema baada ya sheria hiyo kubadilishwa sasa inawataka wasijenge ndani ya Mita 50 kutoka eneo la Reli ambapo inazilazimu jumla ya nyumba 195 kubomomolewa bila kulipa fidia Diwani wa kata ya Sandali Wilibard Abel Tarimo ameiomba Serikali kusikia kilio cha Wananchi hao kwa kuwa Sheria mpya ya mwaka 1995 inawanyima haki zao Wananchi wa kata hiyo ambao wameishi katika eneo hilo zaidi ya miaka 12,hata hivyo Sheria ya Ardhi nchini inasema mtu aliyejenga na kukaa zaidi ya miaka 12 bila kupewa notice hanaki na eneo hilo unapomuhamisha anahaki ya kulipwa fidia Wananchi hao wameelekeza kilio Chao kwa Rais wa awamu ya Tano Mhe John Pombe Magufuli ili awasaidie kupata haki zao kwa madai kuwa wapo hapo tangu enzi ya Baba wa Taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere na kusema Wazazi wao ndio walioshiriki kujenga Reli hiyo pia ndio Walinzi wa Miundombinu ya Reli baada ya kujenga Nyumba zao pembezoni mwa Reli ya Tazara na kuacha Mita 30 zilizowekwa na Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia TAZARA
Mwandishi wa Mtandao huu Sdm Production Media ikamtafuta Mhandisi wa Ukaguzi wa TAZARA Richard Festo ambaye amekiri kuwepo kwa Sheria mbili ya mwaka 1975 na 1995 ambayo inatumika sasa hata hivyo amewataka walalamikaji kuendelea kuyatunza maeneo ya Reli wakati wakiangalia jinsi ya kuwapatia haki zao.
MR.UK KUNGA KIWANDA CHA MAJOKOFU PWANI
-
Meneja Mtendaji wa Kampuni ya Mr.UK Deo Joachim Kusare akionesha jiko la
gesi moja ya bidhaa babdani hapo huku anayeahuhudia ni Meneja Masoko wa
Hotel ...
Siku 2 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni