WASIFU WA ALIYETEULIWA KUWA MKUU WA JESHI LA POLISI, SIMON SIRRO

Rais Dkt Magufuli juzi Mei 28, 2017 alimteua na jana, Mei 29, 2017 alimuapisha Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro ambapo amechukua nafasi ya Ernest Mangu ambaye kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu atapangiwa kazi nyingine.
Simon Sirro ambaye awali alikuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam amekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi wa 10 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mwisho wa makala hii tutawaorodhesha wengine waliomtangulia kushika wadhifa huo.
Simon Nyakoro Sirro alizaliwa eneo la Kiabakari wilaya ya Butiama mkoani Mara mwaka 1963.
Kuhusu elimu yake, Simon Sirro alisoma Shule ya Sekondari ya Ilboru jijini Arusha na Tosamaganga kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu kusoma Shahada ya awali katika Sheria.
Sirro amesoma pia seminari (masomo ya upadri) na kufikia ngazi ya juu kabla ya kuacha na kujiunga na Jeshi la Polisi.
Kamanda Sirro alisema kuwa kama isingekuwa baba yake basi leo yeye angekuwa ni Padri wa Kanisa Katoliki kwani ndiyo ndoto yake kubwa, lakini baada ya wazazi wake kumkatisha ndipo alipojiunga na jeshi hilo.
Unajua wazazi kule kwetu Musoma walikuwa hawakuelewi usipooa. Mzazi aliona mimi ni kijana mkubwa akasema haiwezekani,” alisema Sirro alipofanya mahojiano na Mwananchi kipindi cha nyuma.
Sirro amewahi kuwa Mkuu wa Upelelezi Kituo cha Polisi Buguruni mwaka 1998, Mkuu wa Upelelezi Tarafa ya Magomeni kwa miaka 5 na Mkuu wa Upelelezi Msaidizi Mkoa wa Tabora.
Mwaka 2002 alikuwa Mkuu wa Upelelezi Msaidizi Mkoa wa Dar es Salaam akiwa ni msaidizi wa Abdallah Zombe.
Sirro ni Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam wa tatu ambapo aliteuliwa na Rais Dkt Magufuli Februari 15 mwaka 2006 akichukua nafasi ya Suleiman Kova aliyeshika wadhifa huo tangu mwaka 2008. Kabla ya Kova aliyekuwa akiongoza Kanda Maalum ya Dar es Salaam ni Alfred Tibaigana.
Wakati Suleiman Kova akiongoza Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Sirro alikuwa msadizi wake ambapo baadae alirithi mikoba yake.
Kabla ya kuongoza Kanda Maalum Dar es Salaam, Sirro amewahi kuwa Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Tanzania. Moja ya opersheni kubwa alizowahi kuongozi ni Operesheni Kimbunga dhidi ya wahamiaji haramu mwaka 2012.
Lakini pia, Simon Nyakoro Sirro amewahi kuwa Kamanda wa Polisi wa Mikoa mbalimbali ambayo ni Tanga, Mwanza na Shinyanga.
Wakuu wengine wa Jeshi la Polisi ni;
1. Elangwa Shahidi (1964-1970), alistaafu.
2. Hamza Azizi (1972-1973), aling’olewa na Mwl. Nyerere kwa matumizi mabaya ya madaraka.
3. Samwel Pundugu (1973-1975).
4. Philemon Mgaya (1975-1980), aliachishwa kazi kwa manufaa ya umma.
5. Solomoni Liani (1980-1984), alihitimisha kipindi cha mwisho cha Mwl. Nyerere.
6. Harun Mahundi (1984-1996), alistaafu.
7. Omari Mahita (1996-2006), alistaafu.
8. Said Mwema (2006-2013), alistaafu.
9. Ernest mangu (2013-2017), atapangiwa kazi nyingine, na
10. Simon Sirro (2017-) yupo madarakani.
Mkuu wa Jeshi la Polisi, Simon Nyakoro Sirro ameoa mke mmoja na ana watoto wanne.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List