Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao
cha NEC, mjini Dodoma leo mchana. Kushoto ni Katibu Mkuu
wa CCM Abdulrahman Kinana.
|
BASHIR NKOROMO, Dodoma
HALMASHAURI
Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo imemamliza kikao chake cha siku
tatu chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete ikiwa imeridhia
mapendekezo kadhaa ya Kamati Kuu ya CCM, ikiwemo kumfuta uongozi Mbunge
wa jimbo la Mjini Magharibi, Zanzibar, Mansor Yusuf Himid.
Kikao
hicho pia kimeridhia, uteuzi wa Makatibu wateule wapya wa Jumuia za
CCM, za Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Jumuia ya Wazazi na Umoja wa
Wanawake Tanzania (UWT).
Katika
uteuzi huo mapendekezo hayo yaliyofanywa na Kamati Kuu ya CCM, na
kuridhiwa na NEC, kwa upande wa Umoja wa Vijana wa CCM ameteuliwa
aliyekuwa Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro, Sixtus Mapunda na kwa
upande wa Jumuia ya Wazazi ni Mjumbe wa NEC kutoka Pemba, Seif Shabani
Mohamed, huku kwa upande wa UWT akiachwa Katibu Mkuu wa sasa, Amina
Makilagi.
Mapunda
atachukua nafasi iliyokuwa imneshikiwa na Martine Shigela ambaye
ameongoza UVCCM kwa miaka mitano sasa, na Seif Shabani Mohammed kutoka
Pemba akichukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Hamis Suleiman Dadi
ambaye pia amekuwa katika wadhifa kwa miaka mitano sasa.
Pia,
NEC imeridhia mapendekezo ya Kamati Kuu kwa ajili ya kuziba nafasi
Makatibu wa CCM wa mikoa mitatu ya Morogoro, Kaskazini Pemba na Geita
ambayo kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa imekuwa wazi kwa muda mrefu
sasa kutrokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo.
Kufuatia
mapendekezo hayo ya Kamati Kuu, ambayo yameridhiwa na NEC, walioteuliwa
na mikoa yao ikiwa kwenye mabano ni Msaidizi Kitengo cha Uchaguzi, CCM
Ofdisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Romuli Rojas John (Morogoro),
aliyekuwa Katibu Katibu wa wilaya ya Mkinga, Kassim Mabrouk Mbarak
(Kaskazini Pemba) na aliyekuwa Katibu wa CCM Igunga, Mary Maziku
(Geita).
Kuhusu
sakata la madiwani wa Bukoba mjini, CCM imesema suala hilo, linaendelea
kushughulikiwa ambapo baada ya kikao hicho cha NEC, Kamati kuu
iliendelea kukutana na viongozi wa wilaya ya Bukoba, Mwenyekiti wa CCM
na Katibu wa wilaya hiyo.
Mapema
kabla ya kikao cha NEC, Kamati Kuu ilikutana na Mbunge wa Bukoba mjini
Khamis Kagasheki na Meya wa Manispaa ya Bukoba mjini na kuwahoji, wakati
jana Kamati Kuu ilikutana na Mwenyekiti na Katibu wa CCM mkoa wa
Kagera.
Mwenyekiti
wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha NEC, leo Agosti 26,
2013 mjini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoa utangulizi kabla ya Mwenyekiti
wa CCm Rais Jakaya Kikwete (kushoto) kufungua kikao cha NEC, Agosti 26,
2013
Baadhi
ya wajumbe wa NEC, ukumbini. Kulia mstari wa mbele ni Mjumbe wa Kamati
ya Ushauri ya Viongozi wastaafu wa CCM, John Malecela ambaye ni mwalikwa
kwenye kikao hicho.
Mjumbe
wa NEC, Mama Salma Kikwete akiteta jambo na Katibu wa NEC, Uchumi na
Fedha, Zakiah Meghji kabla ya kikao cha NEC kuanza, Makao Makuu ya CCM
mjini Dodoma.
Mjumbe
wa NEC, Dk. Fenela Mkangala na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro wakijadili jambo kabla ya kikao cha NEC
kuanza leo Agosti 26, 2013, Makamo Makuu ya CCM mjini Dodoma.
Wajumbe
wa NEC kutoka Pemba wakiwa nje ya ukumbi kabla ya kikao kuanza. Kutoka
Kushoto ni Hamadi Bakari Ali, Mwinyi Fakih Hassan, Ali Issa Ali, Masoud
Mohammed Abdallah, Seif Shaaban Mohammed na Mussa Fumu Mussa.
0 comments:
Chapisha Maoni