Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Best Man Promotion, Zumo
Makame (katikati) akiwatambulisha mabondia wawili kutoka Malawi,  Chiotcha Chimwemwe (kushoto) na Bgright Mdoka
(kulia) kwa waandishi wa habari tayari kwa mapambano yao ya Agosti 10.
Cimwemwe  atapambana na Cheka wakati
Mdoka atazipiga na Jitu Samia. Mwingine katika picha ni promota wa Chimwemwe,
Steven Msiska. (Na Mpiga Picha Wetu)
Na Mwandishi Wetu
BONDIA
 nyota wa ngumi za kulipwa wa Malawi, Chimwemwe Chiotcha amewasili 
nchini na kutamba atamtwanga bondia alisyekuwa na mpinzani Tanzania, 
Francis “SMG” Cheka katika pambano lao la uzito wa super-middle 
lililopangwa kufanyika Jumamosi kwenye uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Chimwemwe
 ambaye hajawahi kupoteza pambano nchini Malawi zaidi ya kupigwa kwa 
pointi na Cheka Desemba 27 mwaka jana, alisema kuwa amekuja kulipiza 
kisasi huku akiponda matokeo ya awali kuwa Cheka alibebwa sana.
Alisema kuwa hajui ni ushindi wa aina gani atakaoupata kwa bondia huyo, kwani Knock Out (KO) au Technical Knock Out (TKO) utokea
 ulingoni tu na wala si ushindi wa kupangilia. “Nimekuja hapa kushinda 
na wala si vinginevyo, nakuja Cheka amejiandaa sana, sikuridhika na 
matokeo ya awali na ndiyo maana nimeamua kuja kurudiana naye, najua 
nitaibuka na ushindi,” alisema Chimwemwe.
Alifafanua
 kuwa si kweli kuwa kila bondia aliyepigana na Cheka na kushindwa kuwa 
hajui ngumi za kulipwa zaidi ya hofu tu kutoka kwa mabondia hao. Mimi 
nimedhamilia kufanya kweli na ninajua nitashinda, hii ni fursa yangu,” 
alisema Chimwemwe ambaye ni mwanajeshi wa Jeshi la Malawi.
Mkurugenzi
 wa kampuni ya Best Man Promotion inayoaandaa pambano hilo, Zumo Makame 
alisema kuwa maandalizi ya pambano yamekamilika na siku hiyo kutakuwa na
 mapambano makali nay a kusisimua.
Makame
 aliyataja mapambano hayo kuwa, Deo Njiku atawania ubingwa wa Taifa wa 
Shirikisho la Masumbwi la PST dhidi ya Cosmas Cheka, Rashid “Snake Man” 
Matumla atazichana na Maneno “Mtambo wa gongo “ Oswald na bondia 
mwingine kutoka Malawi, Bright Mdoka atazipiga na Jitu Samia.
Mapambano
 mwngine kwa mujibu wa Makame ni Nasibu Mkude atapigana na Juma Kihiyo 
katika uzito wa super welter bout, Juma Afande v Epson (featherweight) 
na  Karim Mandonga dhidi ya Ramadhan Agogo katika uzito wa superwelter.
Siku hiyo kutakuwa na uhuzwaji wa DVD 
mpya kwa ajili ya mafunzo ya mchezo wa masumbwi zitakazokuwa zikisabazwa
 na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 
'Super D'
DVD hizo mpya ni kati ya  
mike tyson vs evander holyfield na felix trinidad vs roy jones jr
Felix 'Tito' Trinidad vs Pernell Whitaker
ambapo dvd hizo zilizo rekodiwa kwa ubora wa hali ya juu kwa ajili ya kutoa mafunzo ya mchezo wa masumbwi nchin
Rajabu Mhamila 'Super D'
Photojournalist at Majira, Business Times
 Mob;+255787 406938 
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania
 
 
0 comments:
Chapisha Maoni