Nguli wa filamuza (Action) nchini Jimmy Master akiwa ameshika
moja ya tuzo yake katika tuzo zilizoandaliwa na kampuni maarufu ya filamu
nchini Steps.
YULE muongozaji na mwigizaji Jimmy Mponda 'Jimmy Master' aliyetikisa na
mfululizo wa filamu za misuko iliyotoka sehemu ya kwanza hadi ya tatu na
baadaye kujiongezea jina lingine akiitwa
J Plus.
Kwa sasa nyota huyo amefunguka kuwa yukombioni kutoa muvi ya mwisho inayoitwa Doble J Final huku ujio huo ukiwa ni wa mwisho kutoka baada ya kutangulia na Doble J sehemu ya kwanza na yapili zilizotoka mwaka jana.
"Mwaka jana nilifanikiwa kukonga nyoyo za mashabiki wa filamu hususani wanaopagawa
na filamu za mapigano na kujawa mambo ya kipelelezi,"alisema J Plus.
Alisema Doble J Final pia ni ujio wake wa filamu nyingine ya mapigano na kuna heka heka za kipelelezi ndani. J Plus aliyezoeleka sasa katika kuonesha ubabe wa kufa mtu , kwa sasa ujio wake huo unao tazamiwa kuingia sokoni mapema tu , mwezi ujao .
Pia amemshirikisha mbabe mwingine katika filamu za mapigano Ibrahim Mbwana 'Bad Boy' na pia wamo nyota wengine katika dulu la filamu kama Charles Magari , Hashim Kambi na Veronica Viankero.

0 comments:
Chapisha Maoni