Wakazi waishio maeneo ya pembezoni ya Dar es Salaam waifagilia Mobile Clinic ya Benki ya NBCMhudumu wa gari la kutolea huduma za afya linalotembea (mobile clinic) la Benki ya NBC, Wilbard Kiria (kushoto) akimpa mtoto Mwanaharusi Salehe dawa ya vitamin A  katika kliniki ya wamama na watoto iliyokuwa ikiendeshwa na wahudumu wa gari hilo katika eneo la Kunduchi Beach nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana. Gari hilo ni moja ya magari matano yaliyotolewa kwa Bodi ya Afya ya Mkoa wa Dar es Salaam ili kutoa huduma za afya bure kwa wamama na watoto maeneo ya vijijini.

Mtoto mkazi wa Kunduchi, Rukia Ramadhani akipimwa uzito katika kliniki ya wamama na watoto iliyokuwa ikiendeshwa na wahudumu wa gari la kutolea huduma za afya linalotembea (Mobile Clinic) la Benki ya NBC mahali hapo nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana. Gari hilo ni moja ya magari matano yaliyotolewa kwa Bodi ya Afya ya Mkoa wa Dar es Salaam ili kutoa huduma za afya bure kwa wamama na watoto maeneo ya vijijini. Anayempimawa pili kulia  ni muuguzi wa gari hilo, Eliza Shayo.

Mhudumu wa gari la kutolea huduma za afya linalotembea (mobile clinic) la Benki ya NBC, Wilbard Kiria (kushoto) akimpa mtoto Pius Cosmas kidonge cha vitamin A  katika kliniki ya wamama na watoto iliyokuwa ikiendeshwa na wahudumu wa gari hilo katika eneo la Kunduchi Beach nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana. Gari hilo ni moja ya magari matano  yaliyotolewa kwa Bodi ya Afya ya Mkoa wa Dar es Salaam ili kutoa huduma za afya bure kwa wamama na watoto maeneo ya vijijini.
Share on Google Plus

About GLORIA MATOLA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Chapisha Maoni

Watch the Video Here

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

Google+ Followers

TANGAZO

My Blog List