Airtel yaipiga jeki Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani Milioni 40/-



Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, DCP Mohamed Mpinga (kushoto) akipokea hundi ya shilingi milioni 40 kutoka kwa Meneja uhusiano wa Airtel, Bw. Jackson Mmbando. Hundi hiyo ilitolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa dhumuni la kudhamini wiki la nenda kwa usalama barabarani linalotegemewa kuanza wiki ijayo.  Anaeshuhudia kushoto ni Kamanda Msaidizi usalama barabarani Bw, Johansen Kahatano.
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, DCP Mohamed Mpinga akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kupokea hundi ya milioni 40 iliyotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa dhumuni la kudhamini wiki la nenda kwa usalama barabarani litakaloanza wiki ijayo.
****************************
Airtel yakabishi hundi ya shilling million 40 kwa Kitengo cha Usalama Barabarani kufanikisha wito wa mwaka huu “Usalama Barabarani unaanza na mimi wewe na sisi sote”.

Dar Es Salaam , Jumanne, Septemba 17, 2013  kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imekabidhi  Kitengo cha Usalama Barabarani kiasi cha shilling milioni 40 katika kuhakikisha elimu kuhusu usalama barabarani inatolewa ili kuthibiti idadi ya ajali za barabarani nchini.

Hundi hiyo imekabidhiwa na meneja mawasiliano wa Airtel Jackson Mmbando kwa mkuu wa wa Kitengo cha Usalama Barabarani Mohamed Mpinga mbele ya waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu za Usalama Barabarani.

Kutangazwa kwa ushirikiano huo ambapo Mkuu wa kitengo cha usalama barabarani Tanzania Kamanda Mohamed Mpinga ametangaza wiki ya nenda kwa usalama barabarani ya mwaka huu itakayozinduliwa rasmi siku chache zijazo huko mkoani Mwanza.

Akiongea wakati wa halfa hiyo mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani Mohamed Mpinga alisema” nachukua fursa hii kuwashukuru wadhamini wakuu wa kampeni ya usalama barabarani kwa mwaka huu kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, kwa kutoa mchango wao wa pamoja na kushirikiana na jeshi la polisi usalama barabarani kufikia malengo kwa kuhakikisha usalama wa raia na kupunguza ajali za barabarani ”

Ajali za barabarani zinaongezeka kwa kasi na kusababisha upotezaji wa nguvu kazi huku zikiacha maafa makubwa kwa taifa, ni jukumu la kila mtanzania kuwa sehemu ya kusimamia na kuzingatia sheria za barabarini huku tukiishi na kutimiza kauli mbiu ya mwaka huu “Usalama Barabarani unaanza na mimi wewe na sisi sote”.

Nachukua fursa hii kuwaaasa watumiaji wa vyombo vya moto kupeleka magari yao kukaguliwa na kuthibitishwa ubora wa kutembea barabarani ili kuhakikisha vyombo vinavyotumika kubeba abiria viko salama na vinakidhi viwango vilivyowekwa kuhakikisha usalama barabarani.” aliongeza Mpinga

Akiongea kwa niaba ya Airtel, meneja mawasiliano wa Airtel Jackson Mmbando alisema “kwa muda wa miaka mitano sasa Airtel tunajivunia kuwa sehemu ya juhudi za kuokoa maisha ya watanzania  na mali zao na tunayo dhamira ya kuhakikisha tunashirikiana na wadau wote wenye wito wa kusaidia usalama barabarani  na jeshi la polisi usalama barabarani kupunguza ajali za barabarini kwani moja ya dhamira ya  Airtel ni moja kati ya shughuli za kijamii tunazozifanya nchini.

Nia na madhumuni yetu makubwa ni kusaidia shughuli zinazofanywa na jeshi la polisi kusimamia na kupunguza matokeo ya ajali za barabarani, kila mwaka kunakua na matukio ya ajali za barabarani ambazo zingeweza kuepukika kama wahusika wangekua na elimu ya kutosha. Hii ndio sababu kubwa na madhumini ya Airtel kuwa mmoja wa washiriki wakuu katika kusaidia kuhamasisha na kutoa elimu itakayofanikisha upungufu wa ajali barabarani kwa muda wa miaka mitano sasa.”.


Airtel kwa mwaka huu imechangia  kuchapisha stika, kutoa elimu kwa kwa waendesha Boda Boda, ashindano ya mpira kuhamasisha vijana pamoja  na kutoa vitu mbalimbali ikiwemo T shirt 500 zenye ujumbe  wa mwaka huu “Usalama Barabarani unaanza na mimi wewe na sisi sote”.

Tunaamini ajali za barabarani zinaweza kuepukika ikiwa kila moja atafanya sehemu yake Mmbando aliongeza.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List