Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto
ambaye pia ni Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry
Silaa akimlaki mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
Mazingira Dkt. Terezya Huvisa alipowasili kukagua kiwanda kipya na cha
kwanza nchini Tanzania cha kuchambua taka (KIKUTA) kilichopo Gongo la
Mboto jijini Dar. (Picha za Zainul Mzige wa Mo Blog).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa akisalimiana na baadhi ya wakazi wa
Gongo la Mboto mara baada ya kuwasili kiwanda cha KIKUTA.
Diwani
wa Kata ya Gongo la Mboto ambaye pia ni Mstahiki Meya wa Halmashauri ya
Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akizungumza machache kabla ya
kumkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa kuznugmza na wakazi wa Kata ya Gongo la Mboto.
Ofisa
Mtendaji wa Kata ya Gongo la Mboto Bw. Alphonce Msenduki akisoma
taarifa ya kiwanda cha kuchambua taka (KIKUTA) mbele ya mgeni rasmi Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa
alipotembelea kiwandani hapo kukagua juhudi zinazofanywa na Manispaa ya
Ilala.
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Gongo la Mboto Bw. Alphonce Msenduki akikabidhi taarifa ya kiwanda hicho kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa.
Mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa akizungumza na wakazi wa
Gongo la Mboto wakati alipotembelea na kukagua kiwanda cha kuchambua
taka (KIKUTA) kilichopo Gongo la Mboto jijini Dar.
Mh. Dkt. Huvisa amempongeza Diwani
wa Kata hiyo ambaye pia ni Meya wa Halamshauri ya Manispaa ya Ilala
Jerry Silaa kwa jitihada zake za kuhamasisha usafi kwenye Manispaa yake
na kuzitaka Manispaa zingine kuiga mfano wa Manispaa ya Ilala ambapo pia
amewahamasisha wakazi wa Gongo la Mboto kutunza Mazingira kwa kupanda
miti ili kukabiliana na manadiliko ya tabianchi yanayopelekea ongezeko
la Joto duniani.
Pichani juu na chini ni Baadhi ya
wakazi wa Kata ya Gongo la Mboto wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa (hayupo pichani).
Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto ambaye pia ni Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa wakati wa halfa hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Gongo la Mboto Bw. Moshi Mwaluko.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa (katikati) akielekea kukagua kiwanda
hicho akiwa amembatana na Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto ambaye pia ni
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa (kushoto) pamoja
na Afisa Usafishaji wa Manispaa ya Ilala Bw. Samuel Bubegwa (kulia).
Mh. Dkt. Terezya Huvisa akiangalia
maji ya michoro iliyopo katika kiwanda hicho inayohamasisha suala
utunzaji wa Mazingira majumbani.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa
wafanyakazi kiwanda hapo namna wanavyotengeza Mbolea kwa kutumia taka
zilizooza.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa akingalia Mbolea iliyozalishwa
kiwanda hapo tayari kwa matumizi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa akikagua kifaa kinachotumika
kuchambulia taka kwa ajili ya kuzalishwa upya kiwandani hapo.
Mratibu wa Jamii na miradi kutoka Bremen Overseas Research and Development Bi. Larissa Duma (kulia) akifafanua jambo kwa Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa
(katikati) alipotembelea na kukagua kiwanda cha KIKUTA. Kushoto ni
Diwani wa kata ya Gongo la Mboto na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala
Jerry Silaa.
Mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa kwenye picha ya pamoja na
Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto ambaye pia ni Meya wa Halmashauri ya
Manispaa ya Ilala Jerry Silaa pamoja wa wafanyakazi wa kiwanda cha
kuchambua taka (KIKUTA).
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa akiagana
na Mratibu wa Jamii na miradi kutoka Bremen Overseas Research and
Development Bi. Larissa Duma.
**************
Na.Mwandishi wetu.
Manispaa
ya Ilala katika Kata ya Gongo la Mboto imezindua kiwanda cha kuchambua
taka chenye uwezo wa kutengeneza Mbolea, Mboji na bidhaa mbalimbali
zitokanazo na taka ngumu na nyepesi.
Kiwanda
hicho awa kilijulikana kama kituo cha kutupia taka (KIKUTA) ambacho
kilijengwa na mfadhili Bremen Overseas Research and Development kutoka
Canada.
Kiwanda
hicho cha kipekee kimetokana na juhudi za wakazi wa Gongo la Mboto na
Kikundi cha Gongo la Mboto Youth Group wakisaidiana na viongozi wao na
Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto ambaye pia ni Meya wa Halmashauri ya
Manispaa ya Ilala Jerry Silaa.
Kiwanda hicho kitatoa ajira kwa vijana ili kujikwamua kwenye lindi la umaskini.
0 comments:
Chapisha Maoni