Nahodha wa klabu ya Anatori, Athumani Selemani(kulia) na Harid Mohamed
wakishindana kulagi wakati wa mazoezi wakijiandaa na fainali za
mashindano ya Pool Taifa yanayotarajiwa kufanyika Mkoani Morogoro
Septemba 19-22,2013 katika ukumbi wa Tanzanite.
Nahodha wa klabu ya Pool ya Anatory,Athumani Selemani akilagi |
Harid Mohamed akicheza
ANATORY WATAMBA KUTWAA UBINGWA WA
SAFARI POOL TAIFA 2013.
MKURUGENZI
wa Klabu ya mchezo wa Pool ya Anatory, Anatory Makasi ametamba kutwaa Ubingwa
wa fainali za mashindano ya Pool Taifa kwa mwaka huu wa 2013.
Anatory
ameyasema hayo leo jioni alipotembelewa na mtandao huu kujua maandalizi yake
kama mwenyeji wa fainali za mashindano ya Safai Pool Taifa 2013, ambayo kwa
mwaka huu yanatarajiwa kufanyika mkoani Morogoro.
Anatory
amesema anakilasababu za kutwaa ubingwa huo kwani amejiaandaa vizuri,alikuwa na
kambi katika mikoa tofauti ikiwemo Dodoma na Taanga na sasa vijana wako kambini
wakiendelea na mazoezi makali kuikabili mikoa 16ikiwakilishwa na vilabu 16
inayotarajiwa kuwasili kuanzia Septemba 15 na 16 mwezi huu.
Alisema
Anatory vijana wako vizuri hawana shida kabisa wanachosubiri ni kukamilisha
adhima yao ya kutwaa Kikombe na na fedha taslimu shilingi 5,000 000/= kama mabingwa wa “Safari Pool National
Championship 3013”.
Kosi kuwajuza
kuwa Morogoro pako swari,amani tele,usalama upo wa kutosha,hali ya hewa nzuri
kabisa hakuna joto hivyo wachezaji wote pamoja, viongozi na mashabiki
wanakaribishwa Morogoro.
Nae Nahodha
wa Klabu ya Anatory,Athuman Selemani alikitaja kikosi chake anachokiongoza kuwa
ni Harid Mohamed,Six Timbulo,Alfan Ngassa,Juma Kassim,Juma Ally,Charles Philipo
na Mussa Mkwanga.Ambapo viongozi ni Mwenyekiti Jackson Philipo,Katibu Mohamed
Makanyaga na Mkurugenzi Anatory Makasi.
0 comments:
Chapisha Maoni