Kaimu
Mkuu wa Huduma za Kibenki kwa kufuata kanuni za Kiislamu (Islamic
Banking) wa Benki ya NBC, Yassir Masoud (katikati) akikabidhi mfano wa
pasi ya kuingilia katika ndege ya kwenda na kurudi makka kwa mmoja wa
washindi wa promosheni ya kushinda safari ya kwenda hijja, Juma Abdallah
Kheri katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika jijini Dar es Salaam
leo. NBC itagharamia gharama zote zitakazomwezesha mshindi huyo pamoja
na mwenza wake atakayemchagua kwenda kuhiji Makka, Saudi Arabia baadae
mwezi Oktoba. Wa pili kushoto ni mke wa Juma, Sina Abdallah bwago
atakayeambatana na mumewe kwenda hijja na kulia ni Meneja Uhusiano wa
NBC, Eddie Mhina.
Kaimu
Mkuu wa Huduma za Kibenki kwa kufuata kanuni za Kiislamu (Islamic
Banking) wa Benki ya NBC, Yassir Masoud (kulia) akikabidhi mfano wa pasi
ya kuingilia katika ndege ya kwenda na kurudi makka kwa mmoja wa
washindi wa promosheni ya kushinda safari ya kwenda hijja, Hajra
Abdulrahman Ally katika hafla ya makabidhiano ilifanyika jijini Dar es
Salaam leo. NBC itagharamia gharama zote zitakazomwezesha mshindi huyo
pamoja na mwenza wake atakayemchagua kwenda kuhiji mjini Makka, Saudi
Arabia baadae mwezi Oktoba.
Kaimu
Mkuu wa Huduma za Kibenki kwa kufuata kanuni za Kiislamu (Islamic
Banking) wa Benki ya NBC, Yassir Masoud (katikati) akizungumza katika
hafla hiyo jijini Dar es Salaam leo.
0 comments:
Chapisha Maoni