Serana Williams atinga robo fainali US Open



Bingwa mtetezi wa mashindano ya US Open kwa upande wa wanawake Serana Williams (pichani juu) ameingia katika robo fainali ya mashindano hayo, kwa kumshinda Sloane Stephens kwa seti 6-4, 6-1.
 Williams sasa atakutana na mchezaji namabri 18 duniani Carla Suarez Navarro kutoka Uhispania, ambaye alimshinda mchezaji nambari 8 Angelique Kerber wa Ujerumani kwa seti 4-6, 6-3 na 7-6.
 "Ubora wa tenesi ulikuwa wa juu sana, Sloane ni mchezaji mzuri sana, na nilihisi hivyo lakini mwisho wa siku ilikuwa mechi ya raundi ya nne na bila shaka ni hisia za robo fainali kuliko nusu fainali," aliseam Williams baada ya mchezo huo wa raundi ya tatu.
Kwa upande wa wanaume, mshiriki wa mwisho kati ya 15 wa Marekani alipoteza, wakati Tim Smyczek, ambaye ni nambari 109 kwa ubora duniani alipopigwa kwa seti 6-4, 4-6, 0-6, 6-3 na 7-5 na Marcel Granollers kutoka Uhispania.
 Hiyo iliyafanya mashindano ya mwaka huu kuwa ya kwanza katika historia, kutokuwa na mwanaume hata mmoja kutoka nchi muandaji katika raundi ya nne.
Andy Murray Andy Murray.
 Granollers ambaye anashika nambari 43 duniani, atakutana na mchezaji nambari moja duniani Novak Djokovic. Bingwa mtetezi Andy Murray, bingwa wa US Open wa mwaka 2001, Lleyton Hewitt, mchezaji nambari 5 Tomas Berdych, Nambari 9 Stanislas Wawrinka na nambari 21 Mikhail Youzhny pia walifanikiwa kusonga mbele.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List