Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro (kulika) akikata utepe kuzindua ofisi
za Makao Makuu ya Benki ya Maendelea Tanzania (TIB) ya Kanda ya Nyanda
za Juu Kusini na Tawi la benki hiyo Mkoa wa Mbeya iliyofanyika jijini
Mbeya jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa TIB, Peter Noni na
Mwenyekiti wa Bodi ya TIB, Prof. William Lyakurwa.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Benki ya Maendeleo Tanzania (TIB), Prof. William Lyakurwa
(kushoto), akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa ofisi za Makao Makuu
ya TIB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Tawi la benki hiyo Mkoa wa Mbeya
iliyofanyika jijini Mbeya. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,
Abbas Kandoro na Mkurugenzi Mwezeshaji wa TIB, Peter Noni.
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro (katikati) akijaza fomu ili kufunguliwa
akaunti ya Benki ya Maendeleo Tanzania (TIB) Tawi la Mbeya, katika
hafla ya ufunguzi wa ofisi za Makao Makuu ya TIB Kanda ya Nyanda za Juu
Kusini pamoja na tawi hilo Mkoa wa Mbeya iliyofanyika jijini humo. wa
pili kushoto ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa TIB, Peter Noni na anayeongea
naye ni Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi.
.ilianzishwa mwaka 1970 ina takribani miaka 40 kwenye huduma za kifedha
.sasa kuwekeza kwenye miundombinu ya reli, mawasiliano na barabara
.Benki ya wanyonge, mafanikio kichelee, wakulima nao kunufaika
Baada
ya kujiendesha Kwa faida Kwa takribani muongo mmoja, Benki ya Maendeleo
Tanzania (TIB) iliyoanzishwa mwaka 1970 Kama Taasisi ya Maendeleo ya
fedha, Development Finance Institution (DFI), TIB inakusudia kuanza
kuwekeza katika miradi mikubwa yenye kuleta matokeo makubwa na kuendana
na kauli mbiu mpya ya Serikali “Matokeo Makubwa sasa” (Big Results Now).
Baada
ya kufanya kazi Kama taasisi ya maendeleo ya fedha Kwa miaka 25, TIB
ilikuja kubadilishwa na kuwa benki ya uwekezaji (Tanzania Investment
Bank) ili kuongeza uwezo wake wa kukabiliana na changamoto za mabadiliko
ya soko hapa nchini.
TIB
lengo lake kuu ni kutoa Fedha na huduma za uwekezaji na maendeleo
katika Nyanja mbalimbali kama vile kilimo kupitia dirisha lake maalum la
kukopesha wakulima wadogo wadogo (Special Agriculture Window), mikopo
kwa wafanyabiashara na watu wa kipato cha chini ili kuweza kuinua maisha
yao na kuondokana na umaskini.
Kusoma makala hii kwa kina ingia hapa
0 comments:
Chapisha Maoni