Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communications, Maria
Sarungi akizungumza katika uzinduzi wa mashindano ya mwaka huu ya Miss
Universe Tanzania ambayo yamepangwa kufanyika kwenye ukumbi wa
Makumbusho ya Taifa Ijumaa. Kushoto ni mratibu wa mashindano hayo,
Mwanakombo Salim na kulia ni mwakilishi wa kampuni ya Fastjet, Gean Uku.
Warembo
15 wanaowania taji la Miss Universe Tanzania wakiwa katika picha ya
pamoja mara baada ya kutambulishwa na waandaaji. Warembo hao watapambana
Ijumaa kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Ijumaa.
Na Mwandishi Wetu
MASHINDANO
ya kumsaka mrembo wa Miss Universe Tanzania yatafanyika Ijumaa kwenye
ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Posta kwa kushirikisha jumla ya warembo
15.
Warembo
hao kwa sasa wapo kambini kwenye hotel ya Urban Rose wakijifua kuwania
tiketi ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa
yaliyopangwa kufanyika mjini Moscow, Russion Novemba 9 mwaka huu.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Compass Commuications, Maria Sarungi aliwataja warembo
hao kuwa ni Aziza Victoria, Irene Nsiima, Betty Boniface, Kundi
Mlingwa, Mariam Ngwangwa na Naomi Kisaka.
Wengine
kwa mujibu wa Maria ni Glady Msemo, Salsha Lukiko, Upendo Dickson,
Vestina Mhagama, Angela Lutataza , Consolata Mosha, Clara Noor, Agnes
Thobias, Dinah David n Clara Noor.
Alisema
kuwa warembo hao wamepata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania baada ya
kupita katika mchujo wao walioendesha katika mikoa nane ya Tanzania
Bara. Mikoa hiyo ni Mwanza, Arusha, Mtwara, Manyara, Mbeya, Dodoma,
Kilimanjaro na wenyeji Dar es Salaam.
Alifafanua
kuwa lengo lao kubwa ni kupata mshindi ambaye atailetea sifa Tanzania
kama ilivyokuwa kwa Flaviana Matata mwaka 2007 na kuingia katika hatua
ya sita bora nchini Mexico. Mashindano hayo yamedhaminiwa na TANAPA,
Fastjet, Mohamed Enterprises (MetL), Coca-Cola, Missie Popular Blog,
Healthy Beauty Clinic, Beauty Point, Sia Couture, Seif Kabelele Blog,
AZH Photography.com na Adams Digicom.
Mrembo
ambaye kwa sasa anashikilia taji ni Winfrida Dominique. Warembo wengine
waliopita wa ambao hawakuweza kufurukuta katika mashindano ya kimataifa
ni Amanda Ole Sulul (2008), Illuminata James (2009), Hellen Dausen
(2010) na Nelly Alexandra Kamwelu (2011).
0 comments:
Chapisha Maoni