MFUKO WA PENSHENI WA PSPF WAZINDUA MPANGO WA HIARI

Wadau mbalimbali wakiwa wanapata chakula kilichoandaliwa na mfuko wa pensheni wa PSPF kilichoandaliwa kwa ajili ya semina ya mpango wa uchangiaji wa hiari katika mgahawa uliopo Golden Jubilee Front Tower gorofa ya 21. 
 Mwanamitindo flavian matata pamoja na msanii wa filamu lulu michael akifafanua kwa undani zaidi mpango huo wa uchangiaji wa hiari kwa wadau waliofika.Mpango huo uliendeshwa na mfuko wa pensheni wa PSPF.
 Wadau mbalimbali wakifuatilia kwa umakini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Uwendeshaji nd.Francis A.M.Mselemu.
Kaimu Mkurugenzi wa uwendeshaji nd.Francis A.M.Mselemu akiwasalimia msanii lulu na mwanamitindo flavian katika semina ya uchangiaji wa hiari chini ya mfuko wa pensheni wa PSPF.
Mtaalamu wa mambo ya kijamii wa mfuko wa pensheni wa PSPF kushoto akibadilishana mawazo na afsa habari wa PSPF kulia kuhusiana na mpango wa uchangiaji wa hiari katika semina iliyoandaliwa na PSPF
Msanii wa filamu Lulu michael akiwaeleza wadau mbalimbali waliofika katika semina hiyo kuhusiana na mpango mzima wa uchangiaji wa hiari na jinsi yeye atakavyotumia fursa hiyo pembeni yake ni mwanamitindo flaviani matata.
 Mwandishi wa habari akiuliza maswali kwa afisa wa PSPF hayupo pichani kuhusiana na maswala ya uchangiaji wa hiari.
 Kaimu mkurugenzi akitoa ufafanuzi kwa wasanii na wadau pichani kuhusiana na mpango mzima wa uchangiaji wa hiari katika semina iliyoendeshwa na mfuko wa pensheni PSPF katika mgahawa uliopo katika jengo la Golden Jubilee Front Towers.
 Kocha wa timu ya mpira wa miguu ya tanzania Simba S.C ikifafanua mambo mbalimbali kwa wahandishi wa habari alipokuwa akihojiwa na wahandishi mbalimbali.
Wakuu wa mfuko wa Pensheni wa PSPF wakibadilishana mawazo katika semina ya uchangiaji wa hiari.
Mtaalamu wa mambo ya kijamii wa PSPF akifafanua maswala mbalimbali kuhusiana na mpango mzima wa mfuko huo jinsi ya kujiunga na kuchangia kwa hiari. 

 Maafisa wa mfuko wa pensheni wa PSPF wakifuatilia kwa umakini maelezo ya uchangiaji wa hiari ya mfuko huo.
.PSPF ni taasisi ya hifadhi ya jamii iliyoanzishwa kwa sheria na.2 ya mafao ya hitimisho la kazi kwa watumishi wa umma ya mwaka 1999.Hadi mwaka 2012,PSPF ilikuwa inahudumia watumishi wa serikali kuu wakala wa serikali tu.Majukumu ya mfuko huu ni kuandikisha wanachama ambao hadi kufikia mwez septemba mfuko ulikuwa na wanachama 398,717.Mfuko huu unalipa mafao kwa wanachama ambapo kiasi cha shilingi trilion 1.2 zimelipwa kuanzia mwaka 2004 mpaka juni 2013.Thamani ya mfuko imekuwa kutoka shilingi bilion 30.6 mwaka 2000 na kufikia shilingi trilion 1.25 juni 2013.Pia mfuko umesogeza huduma kwa wanachama kwa kufungua ofisi mikoa 23 ya Tanzania Bara.Vilevile mfuko umeshiriki katika mipango mikubwa ya maendeleo ya nchi kama vile ujenzi wa vyuo vikuu,makazi,kuchangia katika kukuza sekta za viwanda na kilimo.MAFAO YANAYOTOLEWA NA MFUKO:1.Kiinua mgongo.2.Pensheni ya kila mwaka.3.Ulemavu.4.Malipo ya pensheni kwa warithi.5.Msaada wa mazishi.6.Malipo kwa wanachama wanaojititoa kwa sababu za kisheria.Katika kuchangia mfuko,moja ya njia kuu ya mfuko ni michango inayotolewa  kwenye mfuko ni jumla ya 20% ya mshahara ya watumishi na huwasilishwa kila mwezi.Watumishi wa serikali pamoja na wakala wa serikali huchangia 5% ya mshahara wa mwajiliwa na waajili wao huchangia 10%.UBORA WA MAFAO:PSPF inatoa mafao bora kwa kuzingatia mabadiliko ya thamani ya fedha mstaafu kupata mafao yanayoendana na mfumuko wa bei.Mafao hukokotolewa kwa kuzingatia mshahara wa mwisho na muda wa utumishi .vigezo (Computation factors)vilivyopo katika kanuni ya mafao vinazingatia maslahi ya mlipwaji zaidi.KWANINI PSPF INAWEKEZA?1.Kulinda thamani ya michango ya wanachama dhidi ya mfumuko wa bei na changamoto nyingine za kiuchumi.2.Kutimiza ahadi ya kutoa mafao yaliyo bora kulingana na fomula yetu ambayo ni bora kwenye sekta.3.Kuchangia maendeleo ya taifa na watu wake.4.Kuchangia kuboresha huduma za jamii.Katika uwekezaji kuna mambo muhimu ya kuzingatia kama Usalama,Ujazo wa fedha (Liquidity),Faida,na Jukumu katika kukuza uchumi wa nchi na jamii kwa ujumla.PSPF INAONGOZA KWA UBORA WA MAFAO,Mfuko unawaomba wote mjiunge na mpango wa uchangiaji wa hiari na muhamasishe Watanzania kujiunga ili waweze kunufaika na utaratibu wa kukopa nyumba kwa riba nafuu..........................PSPF---------TULIZO LA WASTAAFU.
Share on Google Plus

About GLORIA MATOLA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Chapisha Maoni

Watch the Video Here

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

Google+ Followers

TANGAZO

My Blog List