KALAMA NYILAWILA KUZIPIGA NA KAMINJA RAMADHANI


BONDIA Kalama Nyilawila akifanya mazoezi kabla ya mpambano wake na Kaminja Ramadhani picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


BONDIA Kalama Nyilawila atapanda ulingoni jumapili ya novemba 10 katika ukumbi wa Zulu Paradise pugu kilumba kupambana na Kaminja Ramahani mpambano huo wa Raundi 6 utakaopigwa kabla ya mpambano mkubwa 

kati ya Shabani Kaoneka 'BSS' na Said Mbelwa 'Moto wa Gesi' awajaoneshana kazi katika mpambano wao wa raundi 8 

akizungumzia mpambano huo kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini ambaye ni mratibu wa mpambano huo Rajabu mhamila 'Super D' amesema mpambano huo ni mahususi kwa wakazi wa vitongoji vya pugu ,chanika,ilala na jiji la Dar es salaam kwa ujumla 

utakaowakutanisha mabondia mbalimbali ambapo watapigana katika mapambano ya utangulizi bondia Chirambo Hemed atavaana na Sharif Mzezele uku Adamu Ngange akioneshana kazi na Shabani Mtengela 'Zunga Boy' ,Hamza mchanjo atamenyana na Tonny King mpambano mwingine utawakutanisha Twaribu Mchanjo atakaepambana na Mohamed Kashinde,Said Uwezo na Sindano Paul

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Floyd Mayweathar,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo huo vitakaokuwa vikitolewa na Super D kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha ngumi maeneo ya Pugu Kilumba
Share on Google Plus

About GLORIA MATOLA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Chapisha Maoni

Watch the Video Here

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

Google+ Followers

TANGAZO

My Blog List