Kampuni ya Ijumba Enterprises inatarajia kuzindua mradi wa Safari Salama {Safer Journey} katikati ya mwezi November, 2013.
Mradi
huu unalenga waendesha pikipiki za miguu miwili na mitatu yaani
bodaboda. Mradi unalenga kuwaongezea waendesha bodaboda elimu ya udereva
salama na kuzijua sharia za usafirishaji.
Kampuni
hiyo imegundua kwamba ajali nyingi zinazotokana na bodaboda kwa kiasi
kikubwa husababishwa na waendeshaji wake kutokuwa na elimu ya udereva na
sharia za barabara. Pia, vijana wengi wanapfanya shughuli hizi wako
chini ya umri unaotakiwa au kuruhusiwa kuendesha vyombo vya moto
kisheria na asilimia kubwa hawaja hudhuria mafunzo yeyote ya udereva.
Hili limikuwa tatizo kubwa na chimbuko la ajali nyingi barabarani zinazo
sababishwa na bodaboda.
Kampuni
kwa ushirikiano na Jeshi la Polisi idara ya Usalama barabarani na Chuo
cha Taifa cha Usafirishaji {NIT} inatarajia kutoa mafunzo kwa Wilaya za
mkoa wa Dar es Salaam na Pwani. Mafunzo haya yatakuwa niya kivitendo
zaidi na kuwasaidia wadau wao kuweza kupata lesini na kusajili vituo vya
kuegesha bodaboda zao.
Wadau
mbalimbali wanakaribishwa kwamaana ya wadhamini wa mafunzo hayo kwani
hii ni fursa ya kuisaidia juhudi za serikali na jamii kwa ujumla ya
kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu.
0 comments:
Chapisha Maoni