Damas Makangale, Mhariri MOblog
WAZIRI
Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwa mara nyingine tena ameibuka na
kauli ambao alishawahi kuitoa huko nyuma ya viongozi wa Serikali ya
awamu ya nne kushidwa kuchukua uamuzi mgumu kwa maslahi mapana ya taifa.
Lowassa
alitoa kauli hiyo mjini Dodoma katika kikao cha bunge kinachoendelea
akisema nchi inakosa viongozi jasiri wenye kusimamia utekelezaji wa
mambo waliyoamua katika Nyanja mbalimbali za maendeleo.
“wananchi,
wanasiasa, wabunge, viongozi wanalalamika hatuwezi kuwa na jamii ya
kulalamika lazima mtu mmoja ajitokeze na kufanya maamuzi magumu lazima
ajivishe joho la ujasiri ili mambo yaende,’ amesema Lowassa
Amesema
nchi ina tatizo kubwa la uswahili mwingi wa kukaa na kushidwa
kutekeleza mambo yaliyoamualiwa kwenye vikao kiasi cha kufanya kila mtu
kulalamika kwa wakati wake
Lowassa
amesema kuwa hata matokeo makubwa sasa au “Big results Now” haiwezi
kutekelezwa kwa sababu ya uswahili na mazingira ya hapa Tanzania na
Malaysia ni tofauti hapa ni uswahili tu ndio unaosumbua taifa letu
lishindwe kusonga mbele.
“Tukishakubaliana
mambo ni lazima yafanyike. Ni lazima tuondokane kuwa nchi ya kulalamika
kuanzia kiongozi wa juu mpaka mwananchi,” alisisitiza
Sisi
katika Moblog tunaungana na Lowassa katika kutekeleza mipango ya
serikali kama ilivyopangwa bila woga wala kigugumuzi lazima viongozi
wote waliopewa dhamana ya kuongoza waongoze kwa vitendo waache uswahili
ili taifa liweze kusonga mbele.
Tunakubaliana
naye kwa sababu, siku za hivi karibuni tumeona wamiliki malori
wakikataa kulipa tozo ya asilimia tano kwenye mizani ya serikali wakati
sheria ya ongezeko la asilimia hizo tano lilipitishwa na bunge na waziri
mwenye dhamana John Pombe Magufuli alikuwa sahihi kwa kusimamia sheria
lakini kawa kawaida Magufuli alipigwa stop na viongozi wake kwanini?
Sheria za nchi hazifuatwi yale yale uswahili.
Lowasa
ambaye ni mbunge wa Monduli (CCM) amesema kuwa ni vema serikali
ingekuwa na mipango michache yenye kutekelezeka na tija kwa taifa.
Aliongeza
kuwa kama angekuwa kiongozi wa serikali angejikita kwenye vipaumbele
vitatu ambavyo ni ajira, Reli ya Kati na elimu kuliko kuwa na vipaumbele
vingi visivyotekelezeka.
Alibainisha
kuwa tatizo kubwa linaloifanya serikali ishindwe kufanya vizuri kwenye
maeneo mbalimbali ni kujiwekea vipaumbele vingi huku rasilimali zake
zikiwa chache na wakati mwingine zile zinazopatikana hazitumiwi vizuri.
0 comments:
Chapisha Maoni