Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na
Uhifadhi Hati toka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Thomas Willium
akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu zoezi la uchukuaji wa
alama za kibaiolojia linaloendelea katika jiji la Dar es Salaam,zoezi hili
limeshakamilika katika wilaya ya Ilala na pia lipo katika hatua za mwisho
katika wilaya ya Temeke na baada ya hapo litahamia wilaya ya Kinondoni,Kulia ni
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi.Zamaradi Kawawa.
Meneja Mifumo ya Uchambuzi ya Kompyuta wa
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Bw. Mohamed Mashaka akieleza kwa
waandishi wa habari(hawapo pichani) utaratibu wa kuweka majina kwenye mbao za
matangazo ya vituo vya usajili ili wananchi waweze kuhakiki usahihi wa majina
yao.Kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhifadhi Hati toka Mamlaka
hiyo Bw. Thomas Willium
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhifadhi
Hati wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Thomas Willium akiwaonyesha
waandishi wa habari (hawapo pichani) kifaa cha kuchukulia alama za vidole (mobile
enrolment unit).Wakati wa mkutano uliofanyia katika ukumbi wa Idara ya
Habari(MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam. Picha
na Hassan Silayo-MAELEZO
0 comments:
Chapisha Maoni