Meneja
Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)
Bi. Eunice Chiume akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mpango wa
Shirika hilo kuendelea kutatua changamoto za makazi kwa wanachama wake,wakati
wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Leo Jijini Dar
es Salaam.Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi Zamaradi
Kawawa. Picha na Hassan Silayo-MAELEZO
********************************************
Na Georgina Misama
Shirika la Taifa la hifadhi ya jamii (NSSF)
linaendelea na mikakati wa kutatua changamoto za makazi kwa wanachama wake.
Hayo yamesemwa na Meneja Uhusiano na Huduma kwa
Wateja wa shirika hilo Eunice Chiume wakati wa mkutano na waandishi wa habari
leo Jijini Dar es Salaam.
Eunice alisema kuwa
kutokana na kuwepo kwa hitaji kubwa ya
makazi shirika limejipanga kukabiliana na changamoto hiyo kwa kuendelea kujenga nyumba za bei nafuu zitakazouzwa kwa
wanachama wake ili kuweza kuwapatia makazi ya kudumu.
“baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza naya pili
ya ujenzi wa nyumba 297, NSSF tumeona kuna haja ya kuendelea kukukabiliana na
hali hii kwa kuanzisha awamu ya tatu ya mradi wa nyumba za bei nafuu
itakayohusisha ujenzi wa nyumba 900 zitakazo gharimu takriban shilingi bilioni 23.” alisema Eunice.
Aidha Eunice
aliongeza kuwa kuanzia November 11 mwaka huu Shirika linatarajia kuanza kutoa
fomu za maombi ya kununua viwanja 498
vilivyopimwa katika eneo la kiluvya A madukani, viwanja hivyo vitauzwa kwa
ushirikiano wa shirika na Halmashauri ya wilaya ya kisarawe, ambapo eneo hilo litakuwa makazi mapya nay a kisasa
litakalokuwa na huduma muhimu za kijamii.
Viwanja
hivyo vitauzwa kwa wanachama wa NSSF na jamii kwa ujumla kwa bei inayoanzia Shilingi
15,000 hadi Shilingi 20,000 kwa mita ya mraba kulingana na matumizi.
0 comments:
Chapisha Maoni