REDDS MISS TANZANIA 2013 HAPPINESS WATIMANYWA AALIKWA NCHINI UGANDA KUSHIRIKI MAONYESHO YA MAVAZI.
 
Mrembo wa Taifa Redds Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa yuko Kampala Uganda kwa mwaliko rasmi kutoka kampuni ya Arapapa Fashion House & Design ya nchini Uganda.
 
Redds Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa atakuwepo nchini Uganda kwa muda wa siku 5 hadi tarehe 9 Novemba 2013 anatarajiwa kurejea nchini.
 
Akiwa nchini Uganda ataungana na warembo wengine kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, Kenya, Rwanda, Burundi na wenyeji Uganda.
 
Pamoja na mambo mengine warembo hao watahusika pia katika kazi za jamii na baadaye kupanda jukwaani pamoja katika onyesho la mavazi lililoandaliwa na Kampuni hiyo.
 
Kampuni ya Arapapa imekuwa ikifuatilia kwa karibu mashindano ya urembo ya Miss Tanzania tangu mrembo Happiness  anyakue taji na waliazimia kumualika mrembo huyo kutembelea Uganda, jambo ambalo wamelitimiza.
 
Redds Miss Tanzania 2013 ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa  Shahada ya Juu katika Chuo cha Strathclyde  nchini Scotland, ameamua kuahirisha masomo yake kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi hapo atakapovua taji mwishoni mwa mwaka 2014.
 
Mrembo Happiness Watimanywa atawakilisha Tanzania katika mashindano ya urembo ya dunia hapo mwakani.
Share on Google Plus

About GLORIA MATOLA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Chapisha Maoni

Watch the Video Here

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

Google+ Followers

TANGAZO

My Blog List