Mama Tunu Pinda akikaribishwa kufunga maonyesho ya wiki ya Wakinamama Wajasiriamali na Mratibu wa Kitaifa wa Programu ya kuendeleza wajasirimali wanawake Tanzania kutoka ILO, Noreen Toroka. kushoto kwa Mama Pinda ni Mwenyekiti wa MOWE, Bi Elihaika Mrema na
Mke
wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akifunga rasmi Maonyesho ya Wanawake
Wajasirimali (MOWE) katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam,
maonyesho hayo ya wanawake wajasiriamali yalikuwa ya wiki nzima ambapo
wakinamama wanapata nafasi ya kuonyesha na kuuza bidhaa mbalimbali
Usindikaji, Mvinyo, Batiki kwa wakazi wa jijini.
Mratibu
wa Kitaifa wa Programu ya kuendeleza Ujasiriamali kwa wanawake Tanzania
toka Shirika la Kazi Duniani (ILO) Noreen Toroka akizungumza wakati
hafla ya kufunga maonyesho hayo ambapo amesema wiki nzima ilikuwa ni
maonyesho wanawake toka sehemu mbalimbali nchini Bara na Visiwani
wamepata wasaa wakubadilishana mawazo na mbinu za Kibiashara.
Mwenyekiti
wa Kamati ya MOWE, Mama Elihaika Mrema akizungumza wakati wa kufunga
maonyesho hayo ya Wajasirimali wakinamama jijini Dar es Salaam.
Mama Tunu Pinda akitembelea baadhi ya mabanda katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar.
Mama Tunu Pinda akipata maelezo kwa mmoja wa Wajasirimali Wanawake walioshiriki maonyeshio hayo.
Mgeni rasmi Mama Pinda akikabidhi vyeti kwa mmoja wa washiriki wa maonyesho (Certificate of Participation).
Mgeni rasmi Mama Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wenyeji Wake na viongozi wa MOWE.
Mama Tunu Pinda akiserebuka na baadhi ya Wanawake Wajasiriamali wakati wa sherehe za kufunga maonyesho hayo. .Watanzania wahimizwa kununua bidhaa zinazotengenezwa na wazawa
Na Damas Makangale, MOblog
WANAWAKE
Wajasiriamali nchini wameaswa kuzingatia umuhimu wa ubora kwenye bidhaa
zao wanazozalisha kwa kuzingatia viwango vya kitaifa na kimataifa ili
kupata soko la uhakika ndani na nje ya nchi. Moblog linaripoti.
Akizungumza
kwenye kilele cha wiki ya Wajasiriamali Wanawake Tanzania (MOWE) Mke wa
Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda amesema wanawake wanaweza kufanikiwa
endapo watazingatia ubora wa vifungashio (Packaging) wanavyotumia kwenye
bidhaa zao.
“Nimedokezwa
kwamba baadhi ya wajasirimali wamejisajili na kupata kiandishi-anuani
yaani Barcodes, hapa Tanzania, mfumo huu umeanza kutumika hivi karibuni
na wajasirimali wengi wameshawishiowa kujiunga ili bidhaa zao ziweze
kutambuliwa kitaifa na kimataifa,’ amesema
Mama
Pinda amesema kwamba watanzania wote wake kwa waume lazima wapende
kununua bidhaa zinazotengenezwa hapa nyumbani ili kuweza kuwainua
wajasirimali wazawa hasa wakinamama kwa kuunga mkono kampeni ya “Be
Tanzanian, Buy Tanzanian” inayohimiza kuwa Mzalendo, Nunua bidhaa za
kitanzania.
Amesema
hata hivyo, kuna baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na baadhi ya vikundi
vya hapa nyumbani bado hazijaweza kumudu ushindani wa soko na kukubalika
kuuzwa kwenye maduka makubwa yaani supermarkets.
Mama
Pinda aliongeza kuwa changamoto nyingine kubwa inayowakabili
wajasirimali wenhi ni kutozingatia viwango vinavyotambulika katika soko
la ndani la nje ili bidhaa za wazawa ziweze kupenya kwenye soko la
kitaifa, kikanda na kimataifa kwa maslahi mapana ya wajasirimali na nchi
kwa ujumla.
“kwenu
akinamama wajasiriamali na wale waliohidhuria wasio wajasiriamali ni
matumaini yangu kuwa mmetumia fursa hii kubadilishana mawazo na kujenga
mitandao ya kusaidiana na kuendelezana,” alisisitiza
Kwa
upande wake, Mratibu wa kitaifa wa Programu ya kuendeleza Ujasiriamali
kwa Wanawake Tanzania kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO) Noreen Toroka
amesema shirika la kazi linafarijika kuchangia katika mipango na
program za serikali za kuchangia ukuaji wa ajira kwa kupitia program za
ILO katika kumuendeleza mjasiriamali mwanamke nchini.
“kwa
takribani miongo miwili ILO imekua ikifanya kazi kuhakikisha
ujasirimali unachangia ajira na kipato kwa kina mama na tunajivunia kuwa
kati ya wadau wengi walio katika kujengea uwezo washirika wetu idara za
serikali, asasi za kifedha na zisizo za kifedha katika kuwainua
wajasiriamali wakinamama Tanzania,” amesema
Toroka
amesema katika kuendeleza wakinamama nchini ILO imetoa mafunzo ya
ujasiriamali kwa wanawake zaidi ya 500 na kuwaunganisha na huduma za
kifedha na wataalamu wa ujasiriamali kwa elimu ya biashara na stadi za
kazi.
“Kupitia
washirika wetu ILO imefikia wakina mama 100 Mkoani Lindi na tunashukuru
wadau wtu WAMA Foundation na program yao ya village savings and loan,
wakinamama hao walipata mafunzo ya ujasiriamali na tunategemea watapata
mikopo nafuu ili waweze kuanzisha, kuboresha na kupanua biashara zao,”
aliongeza.
0 comments:
Chapisha Maoni