EXTRA BONGO YAMREJESHA KUNDINI MASTER B ALIYEKUWA AMETIMKIA TWANGA




Mnenguaji wa kiume wa Extra Bongo, Master B, aliyekuwa ametimkia bendi ya Twanga Pepeta, wa kwanza (kushoto) akiwajibika na wenzake wakati wa moja ya onesho laeo kabla ya kuihama bendi hiyo, ambaye atatambulishwa rasmi kurejea kundini Extra Bongo.


Na Mwandishi Wetu
BENDI ya Muziki wa Dansi ya Extra Bongo ya jijini Dar es Salaam, imemrejesha kundini mnenguaji wake mahiri wa kiume Kassim
maarufu kwa jina la ‘Master B’.

Mnenguaji huyo alitimkia katika bendi ya Twanga pepeta ya jijini Dar es Salaam na kudai kuwa alirubuniwa kufanya hivyo.

Msemaji wa bendi hiyo Juma Kasesa alisema kuwa kuondoka kwa mnenguaji huyo kulifanya idadi ya wanenguaji wa kiume kupungua kutoka watano hadi wanne.

Naye Master B alikiri kurubuniwa na wadau wa Twanga Pepeta hadi kukubali kuhamia huko lakini alieleza kuwa alipofika huko maisha yalikuwa magumu tofauti na alivyotarajia baada kipindi chote alichokaa huko kushindwa kupewa mkataba tofauti na ilivyokuwa matarajio.



“Mimi nimeamua kurudi baada ya kuona mambo magumu Twanga Pepeta na mipango yangu haiendi sawa ,hivyo nimerudi katika bendi yangu ya nyumbani na naahidi nitafanya vyema kama ilivyokuwa hapo awali na kukosea kwa mwanadamu kumeumbwa,”alisema Master B.
Naye kiongozi wa wanenguaji Hassan Mussa maarufu kwa jina la ‘Super Nyamwela’alisema amempokea Master B baada ya kuomba radhi kwa kile alichokifanya na kuiahidi kuendelea kumpa ushirikiano katika kuimarisha safu ya unenguaji.
Alisema alipoondoka Master B kulibakiwa na wanenguaji wanne lakini kwa sasa kuna idadi ya waenguaji watano na kwamba hali imerudi kama ilivyokuwa awali.
Aliwataja wanenguaji wa kiume waliopo kwenye kikosi hiko uwa ni pamoja na Super Nyamwela mwenyewe,Danger boy,Dogo White, Ally Koncho na Master B.
Tayari Master B yupo Geita, Mwanza na Extra Bongo kwa ziara ya wiki moja moja ambapo leo watakuwa wakiukaribisha mwaka mpya wa 2014.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List