Mambo ya Msondo hayoooo... |
Na Mwandishi Wetu
Wafalme wa muziki wa dansi nchini bendi pizani za Msondo Ngoma
“Baba ya Nuziki’ na Mlimani Park Orchestra (Wana Sikinde Ngoma ya
Ukae) watapambana siku ya Krismasi katika viwanja vya TCC Club
Chang’ombe.
Mpambano huo umeandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts na
kudhaminiwa na Konyagi na Nipashe.
Mratibu wa mchuano huo Joseph Kapinga amesema pambano hilo
litakuwa la kusherekea sikukuu ya Krismasi na kufunga mwaka 2013.
Mratibu huyo alisema kila bendi itapiga kwenye jukwaa lake ili
kuondoa malamiko ya kuhujumiwa. Kila bendi itapiga muziki jukwaani kwa muda wa
saa moja kabla ya nyingine kupanda.
Wakongwe wa Sikinde, Abdallah Hema (kushoto) na Rehani Bitchuka |
“Litakuwa ni pambano la aina yake ukizingatia kila bendi ina
vyombo vipya walivyopewa na kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (Konyagi).
Pia tutakuwa na michezo aina mbalimbali ya watoto,” alisema Kapinga.
Alisema mchuano huo utaanza saa nane mchana hadi majogoo.
Wadhamini wengine wa shindano hilo ni pamoja na gazeti la Nipashe,
Saluti5 na CXC Africa.
0 comments:
Chapisha Maoni