Msondo Ngoma |
Na Mwandishi Wetu
Mabingwa wa muziki wa dansi nchini Msondo Ngoma na
Mlimani Park Orchestra “Sikinde” leo mchana zitachuana vikali
katika viwanja vya TCC Club Chang’ombe, Temeke.
Mpambano huo wa kusherekea sikukuu ya Krismasi litakuwa la
kufunga mwaka 2013 na pia litaamua ni bendi gani bora kati ya magwiji hao wa
muziki wa dansi nchini mwaka huu.
Mratibu wa mchuano huo Joseph Kapinga amesema pambano huo
litanzaza saa nane alasiri hadi majogoo.
Kapinga alisema Sikinde wataingia TCC wakitokea Bagamoyo
walipokuwa wakipiga kambi wakati kambi ya Msondo Ngoma imebaki kuwa siri kwa
muda wote.
Mratibu huyo alisema kila bendi litapiga kwenye jukwaa lake
ili kuondoa hujuma.
Kapinga alisema kila bendi itatapewa muda wa saa moja kupiga
jukwaani kabla ya kumpisha nyingine.
Kiongozi wa Msondo
Ngoma Saidi Mabera alisema jana kuwa watapiga nyimbo zao zote kali ili
kuhakikisha wanaibuka kidedea.
Alitaja baadhi ya nyimbo ambazo watazipiga kuwa ni 'Nimuokoe
Nani', 'Zarina', 'Mwanaidi', 'Kanjelenjele', 'Bahati', 'Sesilia', 'Usiue
Usiibe', 'Asha Mwana Seif', 'Kauka Nikuvae', Chuma Chikoli Moto', 'Kilio cha
Mzima', 'Ajali' na 'Suluhu'.
Bitchuka (kulia) na Dede |
Baadhi ya wanamuziki wanaounda Msondo Ngoma ni Shaaban Dede,
Mabera, Abdul Ridhiwani Pangamawe, Athumani Kambi, Saad Ally 'Mashine', Eddo
Sanga, Huruka Uvuruge, Zahoro Bangwe, Ibrahim Kandaya, James
Mawilla, Juma Katundu, Hamisi Mnyupe, Roman Mng’ande `Romario’ na
Hassan Moshi.
Naye
kiongozi wa Sikinde Hamisi Mirambo alijigamba kuwa wataibuka na ushindi mnono.
“Tuna
waimbaji wazuri na hakuna itakachotuzuia kushinda,” alisema Mirambo.
Alitaja
baadhi ya nyimbo ambazo watazipiga kuwa ni 'Selina', Wiki endi', 'Penzi la
Fukara', 'Hiba', 'MV Mapenzi’, 'Supu Umelitia Nazi' na 'Jinamizi la
Talaka'.
Sikinde
inaundwa na wanamuziki kama Hassan Rehani Bitchuka, Hassan Kunyata, Kaingilila
Maufi, Tonny Karama, Shaaban Mabuyu, Habib Abassi, Juma Choka, Ally
Jamwaka, Mbaraka Othman, Hamisi Milambo, Shaaban Lendi, Joseph Benard,
Ramadhani Mapesa na Habibu Jeff.
0 comments:
Chapisha Maoni