Vicky
Mwakoyo ambaye ni Creative Meneja wa kampuni ya Tan Communication
Media inayomiliki kituo cha Radio 5 Arusha akimkabidhi Mlezi mkuu wa
kituo cha Moshono Fundation msaada katika kampeni
ya Ushindi kwa ajili ya kuwafariji watoto yatima na wanaoishi katika
mazingira hatarishi katika vituo jijini Arusha juzi tarehe 26/1213
katika viwanja vya Matongee Carnivo.
KAMPUNI
ya Tan Communication media imetoa misaada ya chakula yenye thamani ya
shilingi milioni moja na laki mbili kupitia kampeni ya Ushindi kwa
ajili ya kuwafariji watoto yatima na wanaoishi katika mazingira
hatarishi katika vituo kumi jijini Arusha.
Akizungumza
wakati wa chakula cha pamoja cha mchana jana Meneja mbunifu wa kampuni
hiyo Vicky Mwakoyo alisema kuwa lengo ni kuwafariji watoto hao ambao
jamii ya watanzania imewasahau.
Mwakoyo
alisema kuwa watanzania wanatakiwa kubadilika na kuwajali watoto
yatima ikiwa ni pamoja na kutenga muda wao kukaa na kucheza nao ikiwa
ni pamoja na kuwapatia zawadi mbalimbali ili wasijione kama ni wapweke
na wameachwa peke yao.
“Watoto
wote ni sawa na watoto hawa hawajapenda ni mapenzi ya Mungu hivyo
tunawajibu wa kutenga muda wetu na kukaa na watoto hawa kama hivi leo
unaona wamefurahi kama watoto wengine wenye wazazi”alisema Mwakoyo
Aidha
aliongeza kuwa ni vyema jamii ikajenga utamaduni wa kuwasaidia watoto
hawa na isiishie misimu ya kipindi cha sikukuu tu kwa kuwa wanamahitaji
ya chakula kila siku.
“Naomba
niiombe serikali kupitia Wizara ya maendeleo ya jamii jinsia na watoto
kuangalia namna ambavyo inaweza kushirikiana na vituo vya kulelea watoto
yatima kwa kuwapatia fungu ili kupunguza ukali wa maisha katika vituo
hivyo kwa kuwa vina mchango mkubwa kwa taifa”alisema meneja huyo
Tukio
hilo liliofanyika katika viwanja vya Matongee Carnivo
limewakutanisha watoto Yatima zaidi ya Mia moja na hamsini ambapo
walipata nafasi ya kushiriki michezo mbalimbali kama kuvuta
kamba,kukimbia kwenye magunia,mashindano ya kula na kuimba muziki.
Vituo
hivyo vilivyopatiwa misaada ni pamoja na Bethlehemu,Moshono
Foundation,Tumain,Mama na Watoto,St.Joseph,Camp Mosses,Kambarage Lemara
na Karama.
0 comments:
Chapisha Maoni