Na Leca Kimaro, Dar
TIMU
ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC kesho
itapambana na timu inayoundwa na wanamuziki wa bendi ya African Stars
(Twanga FC) katika mechi malaum ya kukaribisha mwaka mpya.
Mechi
hiyo imepangwa kwenye viwanja vya Leaders Club inatarajia kuwa na
msisimko wa aina yake ambapo baada ya mechi hiyo, bendi ya African Stars
itatumbuiza jukwaani kwa mujibu wa mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto
Omary.
Majuto
alisema kuwa mechi hiyo itaanza saa 7.00 mchana ili kutoa nafasi kwa
wanamuziki wa Twanga pepeta kupanda jukwaani kutumbuiza nyimbo zao mbali
mbali ikiwa pamoja na mpya mbali mbali zitakazosikika kwa mara ya
kwanza.
Alisema
kuwa wameamua kucheza na Twanga Pepeta kutokana na ushindani uliopo
ambapo katika mechi ya mwisho, Taswa FC ilishinda kwa mabao 3-1. Alisema
kuwa ushindani wa timu hizo mbili ndiyo umepelekea kufanyika kwa mechi
hiyo ambapo awali, timu ya kombaini ya Jogging itapambana na timu ya
makempu ya Twanga pepeta.
Meneja
wa Twanga Pepeta, Hassan Rehani alisema kuwa kiburudani wamejiandaa
vizuri na wanamuziki wake wamepania vilivyo kuanza mwaka vyema ili kutoa
burudani ya aina yake. “Hii ni sehemu ya zawadi ya mwaka mpya na
wanamuziki wamepania kupiga nyimbo zote zilizotamba mwaka 2013 na pia
watakaribisha maombi maalum ya nyimbo kutoka kwa mashabiki.
“Tuna
albamu nyingi na nyimbo kibao zilizotamba, hivyo ni wakati wa mashabiki
kufanya kile wanachokitaka kutoka katika bendi yetu, wamepewa fursa
hiyo nasi tupo kambili kutimiza maombi yao,” alisema.
0 comments:
Chapisha Maoni