Kaimu
Mhandisi wa Maji Manispaa ya Temeke, ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa
Manispaa hiyo, Meckiline Haule (katikati) akikata utepe ikiwa ni ishara
ya uzinduzi rasmi wa kisima cha maji kilichojengwa kwa msaada wa
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa gharama ya sh. mil. 35 katika Zahanati
ya Kibada, Kigamboni, Dar es Salaam juzi. Wanaoshuhudia ni Mganga
Mfawidhi wa Zahanati hiyo, Isabela Ipopo (kushoto),Mwakilishi wa Mauzo
wa TBL, Allen Mwebuga (wa pili kushoto) na Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa
Manispaa ya Temeke, Rumelius Bakilane
Kaimu
Mhandisi wa Maji Manispaa ya Temeke, ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa
Manispaa hiyo, Meckiline Haule (katikati) akipokea ufunguo kutoka kwa
Mwakilishi wa Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Kanda ya Temeke,
Allen Mwebuga (wa pili kushoto) tayari kuzindua rasmi kisima cha maji
kilichojengwa kwa msaada wa TBL kwa gharama ya sh. mil. 35 katika
Zahanati ya Kibada, Kigamboni, Dar es Salaam juzi. Wanaoshuhudia ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Zahanati hiyo, Nassoro Sande (kulia) na Mganga
Mfawidhi wa Zahanati hiyo, Isabela Ipopo.
Mwebuga wa TBL (kushoto) na Bakilane wakifujaza maji kwenye ndoo wakati wa uzinduzi wa kisima hicho.
Mwakilishi
wa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Rumelius Bakilane akimtwisha
ndoo ya maji Mkazi wa Kijiji cha Kibada, Diana Salvatory baada ya
kampuni hiyo kukabidhi kisima cha maji katika Zahanati ya Kibada,
Kigamboni, Dar es Salaam juzi. Kisima hicho chenye uwezo wa kuhifadhi
maji lita za ujazo 1,600 kwa saa uchimbaji umegharimu sh. mil 35
zilizotolewa msaada na TBL.
Mwakilishi
wa Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Kanda ya Temeke, Allen
Mwebuga akimtwisha ndoo ya maji Mkazi wa Kijiji cha Kibada, Hidaya
Mshindo baada ya kampuni hiyo kukabidhi kisima cha maji cha msaada
katika Zahanati ya Kibada, Kigamboni, Dar es Salaam juzi. Kisima hicho
chenye uwezo wa kuhifadhi maji lita za ujazo 1600 kwa saa uchimbaji
umegharimu sh. mil 35 zilizotolewa msaada na TBL.
Wakifurahi baada ya kuzindua kisima hicho
Mganga
Mfawidhi wa zahanati hiyo, Ipopo akitoa shukrani kwa TBL kwa kuwasidia
kisima hicho, hivyo kupunguza kwa asilimia kubwa tatizo la maji katika
zahanati hiyo.
Mkazi wa Kijiji cha Kibada akitoa shukrani wa TBL kwa msaada huo.
Wakazi wa Kibada wakiangalia kisima hicho
Ofisa
Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu akielezea mikakati ya TBL kusaidia miradi
ya maji nchini ambapo kwa mwaka wafedha wa TBL tayari imetenga sh. mil.
450 kwa kazi hiyo.PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
0 comments:
Chapisha Maoni