Mwanamuziki
mkali wa kuandaa na kupangilia muziki mwenye uwezo wa kupiga ala zote
za muziki, kama, Kinanda, Gitaa zote yaani Solo, Bass na Rhythim, na
zaidi katika kukaanga 'Chips', kuzicharaza drams, Thabiti, Abdul,
ameamua kuachana na kazi za kutumwa na badala yake ameamua kuunda kundi
lake jipya la Taarab, linalokwenda kwa jina la Wakali wao.
Akizungumza
na mtandao huu wa www.sufianimafoto.com, Thabit, alisema kuwa kundi
lake hadi sasa lina jumla ya wasanii 13, na linaendelea na mazoezi yake
maeneo ya Kinondoni katika ukumbi wa Way Bar ili kujiweka sawa kwa ajili
ya kuandaa albam yao ya kwanza itakayokuwa na jumla ya nyimbo nne.
Aidha
alisema kuwa katika bendi hiyo iliyo chini ya Meneja wake, Godfrey
Ngowi, hadi sasa imekwishaanza kufanya shoo katika baadhi ya maeneo huku
ikiwa na waimbaji wengi wapya yaani Ma Under Ground, na wapiga vyombo
aliowataja kwa majina kuwa ni Jumanne Ulaya, anayepiga solo, Shomari
Zizu, anayepiga Gitaa la Bass, Omary Alli na Ndage Ndage, wanaopiga
Kinanda.
Bendi
hiyo inatarajia kutambulishwa rasmi mwezi Februari na kuzinduliwa ramsi
mwezi wa nne katika Sikuku ya Pasaka, ambapo itazinduliwa rasmi bendi
hiyo ikiwa ni pamoja na uzinduzi wa Video zake, Albam na Vyombo vipya,
ambapo kila shabiki atakayeingia getini atapatiwa Cd moja ya Audio yenye
nyimbo za bendi hiyo.
Thabiti,
alizitaja baadhi ya nyimbo hizo kuwa ni pamoja na Kalieni Viti Sio
Umbea, Lipo Linalo Kusumbua, Mtu Mzima Hovyo na Subira Haina Kikomo.
ZAIDI BOFYA www.sufianimafoto.com
0 comments:
Chapisha Maoni