Mhifadhi wa Hifadhi ya Taifa Saadani, Ismail Omar, akizungumza na
waandishi wa habari wa Chama cha Habari za Sayansi Tanzania (TASJA), wakati
walipotembelea hifadhi hiyo, mkoani Pwani, wakiwa katika ziara ya kujifunza
kuhusu mazingira na viumbe hai.
Na Mwandishi Wetu, TASJA.
VITENDO vya ujangili katika Hifadhi ya Taifa ya Saadani iliyopo
wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani vimeendelea kupungua siku hadi siku kutokana na
ushirikiano uliopo baina ya wananchi wa kijiji wa Kijiji cha Saadan.
Kauli hiyo imetolewa na Mhifadhi ya hifadhi hiyo idara ya ulinzi
Ismail Omary alipokuwa akitoa taarifa kwa wanachama wa Chama cha waandishi wa
habari za sayansi(TASJA) waliotembelea hifadhi hiyo kujifunza masuala
mbalimbali.
Alisema ikilinganishwa na kipindi cha nyuma, kwa sasa vitendo vya
ujangili hifadhini hapo ikiwemo ya uharibifu wa misitu na uwindaji haramu wa
wanyama, vimepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na wananchi kutambua umuhimu wa
hifadhi hiyo yenye ukubwa wa kilomita za mraba 1100.
Katika ziara hiyo ya mafunzo iliyowezeshwa na Shirika la Elimu,
Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa(UNESCO)waandishi hao walijifunza
masuala mbalimbali yanayohusiana na umuhimu wa hifadhi za Taifa, kuzitunza na
kuziendeleza.
Kutokana na kufanisha mafunzo hayo Mwenyekiti wa TASJA Greyson
Mutembei, aliishukuru UNESCO kwa niaba ya wananchi kwa kuhakikisha wanajenga
wigo mpana kwa wanahabari kuhusu taarifa za mazingira hasa za wanyama na
vioumbe hai.
0 comments:
Chapisha Maoni