WATUMIAJI WA KADI ZA B-PESA WAHAKIKISHIWA USALAMA WA FEDHA ZAO



DAR ES SALAAM, Tanzania
KADI za B-PESA zilizozinduliwa mapema wiki hii, zimeelewa kuwa usalama wake wa fedha za mteja ni wa hali ya juu.

Imeelezwa kwamba wakati uwezekano ni mkubwa kuhamisha taarifa kwa njia ya ki-eletroniki kutoka katika kadi zinazotumia teknolojia ya 'magnetic' ni vigumu kufanya hivyo kwenye kadi ya B-PESA ambazo teknolojia yake ni ya 'cheap' kama ile ya kwenye laini za simu za mkononi.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam, na  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Smart Banking Solutions (SBS) iliyozindua huduma za kadi hizo za B-PESA, Gustav Vermaas, mapema wiki hii.

Amesema watumiaji wa kadi hizo ambazo zina  huduma mbalimbali ikiwemo kuhifadhi fedha, watakuwa na uhakika wa usalama wa fedha zao hata kama wataibiwa au kupoteza kadi.

Vermaas alisema, ikitokea kuibiwa au kupotea kwa kadi, mteja atatakiwa kuikumbuka tu namba ya siri ya kadi yake ambayo itarahisisha kutengenezewa nyingine itakayomuwezesha kuendelea na matumizi huku fedha zake zikiwa salama.

Alisema kadi hiyo imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa, hivyo hakuna haja ya wananchi kuogopa kuitumia kwani ni sawa na kutembea na benki.

“Unapokuwa na kadi hii, unakuwa unatembea na fedha zako, hivyo unapokuwa na shida, unaingia kwenye mashine zilizoingia ubia na benki au mawakala kutoa fedha au kulipia huduma mbalimbali bila matatizo yoyote, ”alisema.

Alisema kwamba, watumiaji wataweza kutumia mashine za ATM za benki mbalimbali zilizoingia ubia, ingawa kutakuwepo mawakala maeneo mbalimbali kwa ajili ya kupata hudama ya B-PESA.

Aidha, alisema B-PESA itatoa huduma kwa kushirikiana na wadau tofauti zikiwemo benki na mawakala kwa lengo la kurahisisha matumizi ya fedha.

“Mtu anayetaka kusajili kadi ya B-PESA, anatakiwa kwenda kwa wakala aliye karibu huku akiwa na simu ya mkononi. Baada ya kumaliza kujisajili atapokea  ujumbe mfupi kwenye simu yake ambao utathibitisha usajili na namba yake ya siri,”alifafanua.

Alifafanua kuwa, matumizi ya kadi ya B-PESA hayana tofauti na zile za ATM za benki zingine, kwani nazo mtumiaji wake atatakiwa kuingiza kadi yake kwenye mashine za B-PESA, hivyo kutakiwa kuhakikisha kiasi unachotaka kulipa au kutoa na kutakiwa kuingiza namba za siri.

“Baada ya kumaliza kuingiza namba ya siri utapata stakabadhi na lazima uhakikishe kuwa stakabadhi ni sahihi na uitunze. Pia, unaweza kujiunga  na mtandao wetu wa kutuma taarifa kwenye simu kila ufanyapo muamala,”alifafanua.

Kadi ya B-PESA inaruhusu kuwa na matumizi mengi ikiwemo uhamisho wa fedha kwenye kadi, kutolea fedha, kuingiza fedha, na kulipia bili,kununua bidhaa na kulipa huduma mbalimbali.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List