KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Abdi Kassim 'Babi' aliisaidia timu yake ya UiTM ya Malaysia kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Johor baada ya kuifungia bao katika mechi ya Ligi Kuu ya nchi hiyo.
Akizungumza kutoka Malaysia kuwa pambano hilo lililokuwa la pili kwa timu yake katika ligi kuu ya Malaysia lilichezwa kwenye uwanja wa Mini UiTM , uliopo mji wa Shah Alam.
"Nashukuru tumeshuka tena dimbani na kufanikiwa kupata sare ya bao 1-1, bao la timu yetu ya UiTM nikiwa nimelifunga mimi, kwa kweli nasijikia furaha sana," alisema Babi.
Babi alisema pambano hilo lilikuwa kali na wapinzani wa Johor walionyesha walitaka kusawazisha makosa baada ya kuanza ligi hiyo Ijumaa iliyopita kwa kulazwa mabao 3-1 nyumbani kwao na PDRM, lakini walifanikiwa kuwadhibiti na kuambulia pointi hiyo moja.
Kabla ya mechi hiyo, Babi aliishuhudia timu yake ikinyukwa mabao 3-2 katika mechi ya Kombe la FA dhidi ya PBDKT T-Team kabla ya kuanza vyema pambano la ligi kwa kuilaza Kuala Lumpur SPA kwa bao 1-0.
Kiungo huyo wa zamani wa timu za Mtibwa Sugar, Yanga, Azam, KMKM na DT Long ya Vietnam alisema timu yao inatarajiwa kushuka tena dimbani Ijumaa ijayo ya (Februari 7) kwa kuumana na kuumana na DRB-Hicom uwanja wa nyumbani kabla ya Februari 10 kuwafuata PBAPP na kucheza nao kwenye uwanja wa Bandaraya mjini Penang.
0 comments:
Chapisha Maoni