* CAF yaruhusu uwanja wake wa Chamazi
Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika CAF leo tarehe 31 Januari 2014 limeupa kibali cha kuchezea mashindanoya kimataifa yanayoandaliwa na CAF uwanja wa Azam Complex Chamazi na kuufanya uwanja wa kwanzaunaomilikiwa na klabu Afrika Mashariki kuruhusiwa kuandaa (ku-host) mashindano makubwa ya vilabu
Kwa mujibu wa barua pepe iliyotumwa leo na CAF kupitia kwa naibu mkurugenzi wa mashindano Bwana Khaled Nassar, Uwanja wa Azam Compex Chamazi umepita vigezo vyote vinavyohitajika na CAF kuchezewa mashindano ya kimataifa hivyo kuanzia tarehe ya leo, uwanja huu unaruhusiwa “kuchezewa mechi za CAF
0 comments:
Chapisha Maoni