Na Andrew Chale, Zanzibar
MAKAMU
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambaye pia ni Rais wa
Serikali ya Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein kesho Jumamosi Januari
26, anatrajiwa kumnadi mgombea wa Uwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki,
Mahmoud Thabit Kombo, katika uchaguzi mdogo unaoendelea kwenye jimbo
hilo.
Katika
tarifa yake, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alisema
kuwa, Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk Shein atakuwa mgeni rasmi
kwenye mkutano huo wa nne wa hadhara kwenye kampeni hizo zinazoendelea
hivi sasa kwenye jimbo hilo.
Na
kuongeza kuwa, Dk. Shein atawahutubia wananchi sambamba na kumnadi,
Mgombea huyo wa nafasi ya uwakilishi, Mahmoud Thabit Kombo, anayewania
nafasi hiyo kwenye jimbo hilo la Kiembesamaki.
Vuai
aliwataka wananchi wa jimbo hilo kujitokeza kwa wingi ilikusikiliza sera
na ilani za chama hicho katika utekelezaji wake iliwakichague chama cha
Mapinduzi kwa misingi imara ya kuwaletea maendeleo.
Aidha,
kwa upande wake, Mahmoud Thabit Kombo aliwaomba wananchi wa jimbo
hilo, kumpigia kura hiyo Februari mbili, ili akawawakilishe kwenye
Baraza la Wawakilishi.
“Nawaomba
Wanakiembesamaki, kutumia fursa ya kipekee ya kunichagua ilikuweza
kuwawakilisha kwenye BAraza, hakika chama chetu ni sikivu na daima kipo
na wananchi katika kuwatetea na kuwaletea maendeleo” alisema, Mahmoud.
Kampeni
za uchaguzi mdogo wa jimbo la Kiembesamaki, zilianza Januari 21, ambapo
zinatarajia kumalizika Februari Mosi, mwaka huu huku wananchi
wakitarajia kupiga kura ya chaguzi huo, Februari mbili.
0 comments:
Chapisha Maoni