Hemba aiangukia serikali, wadau wa dansi



Hemba (kushoto) akiwa na Hassani Bitchuka
MWANAMUZIKI wa bendi kongwe ya muziki wa dansi ya Mlimani Park 'Sikinde', Abdallah Hemba, ameiomba serikali na wadau wa muziki kwa ujumla kusaidia kuupiga tafu muziki wa dansi kwa madai ndiyo kutambulisho halisi cha muziki wa Tanzania
Aidha amewataka wanamuziki wenzake kupendana na kusaidiana katika shida na raha kama wafanyavyo wasanii wa fani nyingine ili kujenga umoja na mshikamano.
Akizungumza na MICHARAZO katika mahojiano maalum, mtunzi na muimbaji huyo, alisema dansi limekuwa likichechemea kutokana na kutopata sapoti ya kutosha kama fani nyingine kitu ambacho alisema mwaka 2014 uwe wa mabadiliko na muziki huo kupewa kipaumbele.
Hemba, aliyewahi kutamba na Mchinga Sound na Super Sikinde Sound, alisema wapo wadau wa muziki huo wamekuwa wakiwaangusha kwa kutoupa kipaumbele katika nafasi zao hasa watangazaji na kuufanya muziki wa dansi hudorore.
Pia alisema ni lazima wanamuziki wa miondoko hiyo wapendane na kusaidiana kusaidia kujenga udugu na mshikamano utakaofanya wasonge mbele katika medani ya muziki nchini.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List