Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Amos Makala ambaye kwa sasa amehamishiwa Wizara ya Maji kama Naibu Waziri akimkabidhi vyeti vya utendaji bora wa huduma za michezo Mkurugenzi wa Masoko Kampuni ya Issere Sports, Abbas Ally Issere katika kongamano la Wasanii lililoandaliwa na Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA),Makala kwa sasa amehamishiwa Wizara ya Maji kama Naibu Waziri (Picha na Mpiga Picha Wetu).
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Issere Sports inayojishughulisha na uuzaji wa vifaa vya michezo nchini ni miongoni mwa wanamichezo, wasanii na awaandishi wa habari 1,000 waliotunukiwa vyeti vya utendaji bora katika fani za michezo kwa mwaka 2013 hadi 2014 katika kongamano lililofanyika ukumbi wa Lamada, Ilala Dar es Salaam.
Katika kongamano hilo ambalo kulitolewa mada mbili za kusaidia jamii ya wanamichezo kujiepuka na matumkizi ya dawa za kulevya, ya pili ikiwa ya maadili bora katika jamii, Kampuni ya Issere ni pekee iliyopata nafasi ya kuwakilisha nyingine zinazojihusisha na uuzaji wa vifaaq vya michezo.
Mkurugenzi wa Masoko wa Issere Sports, Abbas Issere aliyepokea vyeti hivyo kwa niaba ya wanamichezo wengine wa Kampuni hiyo alisema zawadi hiyo ni changamoto kwa wanamichezo kushirikiana pamoja badala ya kubaguana ili kurejesha heshima katika michezo kama ilivyokuwa miaka ya zamani na kutoa mfano kuwa katika riadha ilitawaliwa na Selemani Nyambui, Juma Ikangaa na Filbert bayi.
Kampuni ya Issere Sports ambayo imeingia mkataba wa kuuza jezi za Klabu ya Simba, imekuwa ikiuza na kusambaza jezi hizo nchini na Mashirika ya Umma, Wizara, Halmashauri za Wilaya na mashuleni katika ngazi ya shule za msingi, Sekondari na vyuoni.
0 comments:
Chapisha Maoni