1. Naibu Waziri huyo akipata ushauri kutoka kwa wataalam baada ya kupima uzito, sukari na shinikizo la damu.
1.
Wananchi mbalimbali wakiendelea kupata huduma za
vipimo katika banda hilo.
Ofisa Matekelezo na Uratibu Ainess Bamanyisa akitoa elimu kwa askari polisi waliohitaji ufafanuzi wa huduma zinazotolewa na Mfuko
1.
Wananchi wakiendelea kupata huduma za elimu na
vipimo.
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya
umehudumia mamia ya wananchi wa visiwani Zanzibar wamepata huduma za vipimo na
ushauri wa kitaalam wa kuepukana na maradhi yasiyoambukiza kwenye banda la
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Wakazi hao ni wale waliofika
kwenye maonyesho ya maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar
yaliyomalizika visiwani humo jana.
Uongozi wa mfuko huo umeweka
huduma hizo ambazo zinatolewa bure katika maonesho hayo kwa lengo la kuwasaidia
wananchi kutambua afya zao na kuweza kujikinga.
Vipimo vilivyotolewa katika
banda hilo ni pamoja na vipimo vya urefu, uzito, shinikizo la damu na kisukari.
Mbali na kuhudumiwa, Kaimu
Mkurugenzi wa Mfuko huo, Bw. Hamis Mdee ametoa mwito kwa wananchi visiwani humo
kujiunga na NHIF ili wawe na uhakika wa kupata matibabu popote pale walipo
Tanzania.
“Nitumie fursa hii kuwaomba
sana Wazanzibari kuona umuhimu wa kujiunga na huduma zetu ili muweze kunufaika
na mtandao mkubwa tulionao wa watoa huduma nchi nzima, sisi ni binadamu hatujui
ni lini tutakuwa wagonjwa na tutakuwa wapi lakini hapa fedha unaweza ukawa huna
kwa wkati huo hivyo ni vyema ukawa mwanachama,” alisema.
Alisema kuwa NHIF imesogeza
huduma zake visiwani humo kwa kufungua ofisi ili wananchi na wanachama waweze
kupata huduma kwa uharaka na ukaribu zaidi.
Akizungumza katika banda hilo,
Ofisa Udhibiti Ubora wa NHIF, Dk. Ally Mvita alisema idadi ya wananchi
wanaofika kwa ajili ya vipimo hivyo iliongezeka siku hadi siku.
“Hii inatoa hamasa kwa wengine
kuja kupima lakini pia tunawashauri wote wanaofika bandani kwetu namna bora za
kujikinga na magonjwa hayo yasiyoambukiza,” alisema Dk. Mvita.
Awali Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
NHIF, Hamis Mdee alisema hiyo ni fursa kwa wakazi wa visiwa hivyo kujua afya
zao huku akiwataka kuwatumia vema wataalam hao wa afya.
Kwa mujibu wa Mdee lengo la
NHIF ni kusogeza huduma kwa wananchi wote ili kufikia malengo ya kuwafikia
watanzania wote kwa kuwa afya ni msingi wa maendeleo na uchumi imara.
Mfuko huo unatoa mafao 11 kwa
wanachama wake kupitia watoa huduma waliowasajili katika kuhakikisha wanachama
wao wanapata huduma bora za afya waakati na mahala popote.
Baadhi ya mafao yanayotolewa na NHIF ni gharama za upasuaji, kulazwa, vipimo, dawa mbalimbali, matibabu ya macho, miwani ya kusomea, kinywa na meno, mazoezi ya viungo, mafao kwa wastaafu, vifaa saidizi na ada ya uandikishaji.
0 comments:
Chapisha Maoni