Mwenyekiti
wa Yanga Yusuf Manji amewaomba wadhamini wa klabu hiyo, kuangalia upya
mkataba wa Azam TV, kwani kwake yeye binafsi anauona hauna manufaa kwa
klabu yao ambayo inaingiza zaidi ya mil 300 katika mchezo mmoja akitolea
mfano mchezo kati yao na Watani zao Simba.
Baada ya
kusema hayo, Manji aliwataka wanachama kutoa maoni yao juu ya suala
hilo, ambapo Patric Mandewa kutoka Mwembeyanga aliunga mkono hoja ya
Manji na kusema kuwa, hawaoni faida ya kuchukua mil 100 kutoka Azam TV
wakati wao ni klabu kubwa ambayo inauwezo wa kujisimamia na katika mechi
moja ikapata zaidi ya fedha hizo.
Mbali na
hayo, wanachama wakiongozwa na Tuni Bakar ‘Mama Tuni’ walilazimika
kumpigia magoti Manji ili kumuomba kupangua kauli yake ya kutotaka
kugombea tena, nafasi ya Uenyekiti ambayo bado anaishikilia mpaka sasa
baada ya aliyekuwa Mwenyekiti Loyd Nchunga kujiudhuru.
Licha ya
wanachama hao, kumtaka Manji kupangua kauli hiyo, Manji aliendelea na
msimamo huohuo huku akiwataka wanachama kuachana na hoja hiyo kwani
haina mashiko katika maendeleo ya Yanga kwa kuwa uongozi ni demokrasia,
na kujikuta akiharibu hali ya hewa baada ya kauli hiyo na wanachama
kuanza kuondoka ndani ya ukumbi huo.
Baada ya
wanachama kuondoka, Mc wa Mkutano huo, Bakiri Makere aliwataka wanachama
kutulia huku akisema ‘Yanga Oyeee’ na kujikuta akikosa wa kumjibu kama
ilivyokuwa awali kabla ya Manji kujibu kwa msisitizo kuwa hatagombea
tena kiti hicho.
Uongozi wakili kikosi kuwa dhaifu….
UONGOZI
wa Klabu ya Yanga, umekiri kikosi chao kuwa na uwezo wa mchezaji mmoja
mmoja huku wakidai hiyo ndiyo sababu ya timu yao kutofanya vema katika
michezo mbalimbali ambayo imechezwa hivi karibuni licha ya kuongoza
ligi.
Hayo
yalisema na Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, ambaye aliwaweka
wazi wanachama wa klabu hiyo, sababu za kutimua benchi la ufundi chini
ya Kocha Mkuu Ernie Brandts na msaidzi wake Fred Felix ‘Minziro’.
Sanga
alisema, walifikia hatua hiyo, baada ya kuona benchi la ufundi
linashindwa kufanya kazi na kujikuta wakipanga vikosi kwa mazoeza bila
ya kutazama uwezo wa mchezaji mwenyewe na kuangalia majina.
“Timu ina
wachezaji wazuri lakini ni mmoja mmoja, timu haichezi kitimu ni ngumu
kufanya vizuri, na ndio maana tukachukua hatua hiyo, na huu ni mwanzo
kwani hata wachezaji wenye utovu wa nidhamu atautaangalia jina la mtu
wala nini tunamwajibisha tu,”alisema Sanga na kuongeza kuwa, hata
wachezaji wanaocheza mchangani watawashughulikia.
0 comments:
Chapisha Maoni