Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa watendaji wa Tanroads.
Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa anafuatilia kazi katika moja ya mitambo ya barabara.
Waziri
wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika ukaguzi wa eneo
lililobomolowa na mafuriko ya mvua katika daraja la Mkundi, Dumila
mkoani Morogoro.
Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza mmoja wa madereva wa Lori zinazofanya kazi katika eneo hilo.
Mtambo ukiwa kazini
Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuelekeza dereva wa lori kumwaga mawe sehemu husika.
Muonekano wa Daraja hilo.
Waziri
wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo ametembelea eneo la Dumila
ambako mvua kubwa zinazoendelea kunyesha zimesababisha mafuriko ambayo
yameharibu sehemu ya barabara kwenye daraja la Mto Mkundi mkoani
Morogoro.
Akiwa
katika eneo hilo Waziri Magufuli baada ya kujionea hali halisi
amemwagiza Kaimu Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi Crispianus Ako
pamoja na Watendaji wengine waandamizi kutoka Tanroads na Wizara ya
Ujenzi kuwepo hapo muda wote wakati kazi za kurejesha mawasiliano
zikiendelea ili kuhakikisha kuwa matengenezo hayo yanakamilika kesho
siku ya Ijumaa tayari kwa magari kuanza kupita.
Katika
hatua nyingine Mhe. Magufuli ametahadharisha kuwa magari yanayoruhusiwa
kuzungukia barabara mbadala inayoanzia Dumila kupita Kilosa hadi
Morogoro ni mabasi ya abiria na magari mengine yasiyozidi uzito wa tani
10. “Barabara hii mbadala ya kupitia Kilosa, Melela hadi Morogoro ni ya
mkoa na iko katika kiwango cha changarawe ikiwa na madaraja yenye uwezo
wa kubeba chini ya tani 10 tu, hivyo magari mengine yote yenye uzito
zaidi ya hapo yatabidi kusubiri wakati tukiendelea na jitihada za
kuifungua barabara hii mapema iwezekanavyo” amefafanua Mhe. Magufuli.
Daraja
la Mkundi liko kiasi cha kilometa 65 kutokea Morogoro mjini kuelekea
Dodoma na mikoa mingine ya kati hadi magharibi mwa nchi yetu ikiungana
na nchi jirani za Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya watu wa Kongo.
0 comments:
Chapisha Maoni