MBUNGE WA CHADEMA IRINGA MJINI AMFAGILIA RAIS KIKWETE KATIKA KUHAKIKISHA KATIBA MPYA INAPATIKANA.





Mbunge  wa jimbo la  Iringa Mjini,Mh.Peter Msingwa amefanya mkutano hapo jana katika  viwanja vya Mwembetogwa,  mkoani humo.
Mkutano huo ambao ulikuwa wa kufungia mwaka 2013 ,Msigwa pia aliutumia mkutano huo kwa kuwapongeza baadhi  ya  mawaziri ambao utendaji kazi wao unaonekana kuwa mzuri,akiwemo   Waziri wa Wizara ya Maji na  Naibu Wake ,Waziri wa Ujenzi na  Waziri wa Mazingira  ambao wameonesha  msimamo wa kweli katika  kuwatumikia  wananchi .

katika hatua nyingine  mbunge Msigwa  amemshukia aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema,Zitto  Kabwe na kusema kuwa anatafuta umaarufu binafsi  kuliko  kukijenga chama  chake na  kuwa  hana nia njema  na CHADEMA,hivyo amewataka Wanachadema wa jimbo la Iringa mjini kutomsikiliza huku akibainisha kuwa Mwanachama na Kiongozi mzuri ni  yule ambae  anafanya kazi ya  kukijenga chama chake na  si kujijenga  yeye binafsi.


Amesema  kuwa iwapo  Zitto hatotaka kumsikiliza mwasisi wa Chama  hicho, Mzee Mtei  wala  kuwasikiliza viongozi wa juu wa chama  hicho akiwemo  mwenyekiti wa katibu mkuu, ni  wazi hakitakii mema CHADEMA,na wana Chadema hawana budi kumpuuza kiongozi na mwanachama yeyote mwenye lengo la kuua chama.


Kuhusu rasimu ya Katiba,   Mbunge  Msigwa amempongeza Rais Kikwete  kuwa ameonyesha ushujaa wa hali ya juu  katika kupigania  upatikanaji wa katiba mpya, na  kuwa  iwapo  wabunge wa CCM watapinga  wao kama Chadema  watarudi kwa wananchi   kuhamasisha  kupiga kura ya kuikataa  katiba  itakayopendekezwa na wabunge wa CCM.

Aidha Msigwa ameongeza kusema kuwa atakuwa mstari wa mbele kuikosoa serikali kama itaonekana kuwa na viongozi dhaifu huku akiwataka watanzania kutathimini yale yote waliyofanya mwaka 2013 na kuwatakia kheri ya mwaka mpya.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List