Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya kusambaza vifaa vya umeme wa jua (solar) ya Rex
Energy Bw Francis Kibhisa akizungumza na Wanahabari kutoka vyombo
mbalimbali (hawapo pichani),kuhusiana na uzinduzi na utambulisho wa
teknolojia mpya yenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi na kusambaza
Umeme,mkutano huo umefanyika mapema leo asubuhi kwenye makao makuu ya
ofisi hizo zilizopo mtaa wa Makamba,Gerezani jijini Dar.
Pichani
mbele kushoto ni Ofisa Mauzo wa kampuni ya Rex Energy,Bwa.Medard
Rweikiza pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo,Bwa.Francis
Kibhisa wakiwaonesha na kuwaeleza baadhi ya Waandishi wa Habari namna
moja ya kifaa cha kisasa kabisa chenye uwezo mkubwa wa kuzalisha umeme
kwa kutumia Mwanga wa Jua (Solar).Kwa habari zaidi ingia www.rexsolarenergy.com
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Rex Energy,Bwa.Francis Kibhisa akitoa ufafanuzi
wa namna moja ya kifaa (pichani),kinachotumia teknolojia ya kisasa
katika suala zima la kuzalisha umeme kwa kutumia mwanga wa jua (Solar
Power) mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani),Bwa.Francis
alibainisha kuwa kifaa hicho kina uwezo wa kuwasha vifaa vya ndani kama
vile taa,redio, friji, TV kwa wakati mmoja,na huuzwa kwa gharama
nafuu.Pichani kulia ni Ofisa Mauzo wa kampuni ya Rex Enegy,Bwa.Medard
Rweikiza akisikiliza
Baadhi
ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Rex Energy wakiwa katika picha ya pamoja
mara baada kumaliza mkutano wao na Waandishi wa habari mapema leo
asubuhi.
0 comments:
Chapisha Maoni