Katibu
Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akikabidhiwa fomu ya
kugombea nafasi ya mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa, kutoka kwa Katibu wa
tawi lake la Kidatu 'A' Mtoni, Bakar Hamad Ali. Aliijaza fomu hiyo na
kuirejesha papo hapo.Picha na Salmin Said-Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar
----
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amewataka
wanachama wa chama hicho kufuata taratibu wakati wanapotaka kugombea
nafasi za uongozi ndani ya chama.
Amesema
si halali kwa mwanachama yoyote kupelekewa fomu ya kugombea nyumbani au
ofisini kwake, na badala yake anatakiwa kuchukua fomu hiyo katika tawi
lake au kumtuma mwakilishi wake kufanya hivyo.
Mhe.
Maalim Seif ametoa kauli hiyo katika tawi lake la Kidatu ‘A’ Mtoni,
baada ya kuchukua fomu ya kugombea ujumbe wa mkutano mkuu Taifa.
Amesema
ameamua kuchukua fomu hiyo katika tawi hilo, ili kudhihirisha ukomavu
wa demokrasia ndani ya chama hicho, na kwamba hila mwanachama ana haki
ya kuchukua fomu na kugombea nafasi yoyote anayoitaka ndani ya chama.
Amesema
chama kitahakikisha kuwa chaguzi ndani ya chama zitakuwa za uwazi, huru
na haki, na hakuna atakayependelewa wala kuonewa katika chaguzi hizo.
Amefafanua
kuwa katika kuhakikisha hilo linatendeka, chaguzi za Wilaya
zitasimamiwa na wajumbe kutoka nje ya Wilaya husika, na ikiwezekana
baadhi ya wasimamizi watatoka Tanzania Bara.
Jumla
ya viongozi 20 kutoka Wilaya ya Magharibi wanatarajiwa kuchaguliwa kuwa
wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa, kupitia mkutano mkuu wa Wilaya
unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni, baada ya kukamilika kwa changuzi
ngazi za majimbo.
Maalim
Seif amechukua fomu hiyo ambayo aliijaza na kuirejesha papo hapo mnamo
majira ya saa 6.00 mchana, ambapo alikabidhiwa na katibu wa tawi hilo
nd. Bakar Hamad Ali.
Katika
hatua nyengine, Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar amekemea tabia ya makundi na mitandao ndani ya chama, na kwamba
makundi hayo hayakubaliki ndani ya chama hicho.
Amesema
chama kinaweza kufuta uchaguzi wa ngazi yoyote ya chama iwapo kitabaini
kuwepo kwa kampeni chafu, ikiwa ni pamoja na uwepo wa mitandao,
makundi, pamoja kampeni chafu dhidi ya wagombea wengine.
Ameongeza
kuwa mwanachama pia anayo haki ya kukata rufaa ikiwa hakuridhishwa na
zoezi la uchaguzi, na kwamba rufaa yake itasikilizwa na kutolewa maamuzi
yanayofaa kwa mujibu wa taratibu za chama.
Nae
Mwenyekiti wa Tawi la Kidatu ‘A’ Mtoni bw. Ali Juma, amesema nafasi za
uongozi ndani ya chama hicho ziko wazi, na kila mwanachama ana haki ya
kuomba nafasi yoyote ya uongozi.
Amesema kitu cha msingi ni kufuata taratibu zilizowekwa, ambazo zinatoa fursa ya demokrasia ndani ya chama hicho.
Na
Hassan Hamad
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar
0 comments:
Chapisha Maoni