Katika
ziara hiyo waziri alijionea jinsi tani zaidi ya 1800 za mpunga
uliovunwa na mwekezaji ukiwa umehifadhiwa nje ya maghala kutokana na
kukosekana na soko ndani na nje ya nchi hivyo kufanya kiwanda kuendeshwa
kwa hasara.
Waziri
wa Ardhi,Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka amemtaka Mwekezaji wa
shamba la Mpunga la Kapunga[Kapunga Rice Project]kuachia hecta 1870 za
Kijiji ili kumaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda mrefu.
Rai
hiyo ameitoa alipofanya ziara katika shamba hilo ambalo liliuzwa hecta
7370 badala ya 5500 ambazo ndizo zilizostahili na kuacha hecta 1870
ambazo ni eneo la kijiji kabla ya kukabidhiwa shamba la NAFCO kabla ya
kubinafsisha.
Ziara
hiyo imefanywa na Waziri ili kujiridhisha baada ya kupokea mgogoro huo
kwa muda mrefu bila majibu ya kuridhisha kutoka kwa watendaji wake hivyo
kama Waziri mwenye dhamana lazima atoe majawabu yenye uhakika badala ya
kuolea majibu ofisini.
Profesa
Tibaijuka alikutana na Uongozi wa Serikali ya kijiji kabla ya kukutana
na Mwekezaji na kuhitimisha kwa kufanya mkutano wa hadhara uliofanyika
katika kijiji cha Kapunga ambao pia ulihudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM
wilaya ya Mbarali Matayo Mwangomo,Mkuu wa wilaya ya Mbarali Gulamhusein
Kiffu na wataalam mbalimbali kutoka wilayani na mkoani.
Waziri
Tibaijuka aliwashukuru wananchi wa Kapunga kwa uvumilivu wao kwani
licha ya mgogoro kudumu muda mrefu hawajafanya vurugu zozote hivyo
alimtaka Mwenyekiti wa kjiji hicho Ramadhan Nyoni kudumisha amani na
upendo ili kumaliza mgogoro huo bila uvunjifu wa sheria.
Profesa
Tibaijuka alipata maelekezo ya shamba hilo kutoka kwa mmoja wa
wakurugenzi, Mkurugenzi mtendaji Bwana Justin Vermaak ambaye alimweleza
kuwa suala la kuachia ardhi atakutana na wabia wenzake watano ili kutoa
majibu muda mfupi ujao.
Hata
hivyo Bwana Vermaak alibainisha kuwa shamba hilo linakabiliwa na
changamoto ya wizi wa mbolea na mpunga kutoka kwa baadhi ya wananchi
hivyo kuzorotesha uzalishaji wa mpunga.
Aidha
Vermaak alimwambia Waziri kuwa kuharibiwa kwa miundo mbinu ya mifereji
ya maji kilometa 14 kutoka mto Ruaha kumepelekea kupungua kwa maji
katika shamba hilo hivyo kulazimika kulima chini ya kiwango.
Pia
Bwana Vermaak amemwambia Waziri kuwa wanalazimika kukodisha mashamba
kutokana na kuombwa na wananchi wa Kapunga ingawa hakuwa wazi juu ya
mikataba ya ukodishaji kuokana na mashamba hayo kukodishwa kwa shilingi
2,880,000 kwa plot na kutakiwa kulipa mwekezaji tani 24 hadi 27 za
mpunga baada ya mavuno.
Wananchi
wameonekana kushindwa kumudu gharama za uendeshaji kauli iliyoungwa
mkono na Diwani wa Kata ya Itamboleo mheshimiwa Lwitiko Mwangosi ambaye
amesema kuwa licha ya kulipia shilingi 1,680,000 mwaka jana lakini
hakupata kitu baada ya mwekezaji kuchukukua mpunga wote aliovuna.
Baada
ya kukutana na uongozi wa kijiji na mwekezaji Waziri alihutubia
wananchi na kuwaambia kuwa hivi sasa mgogoro haupo baada ya kumwomba
mwekezaji kuachia hecta 1870 na kuwataka wananchi kuwa na subira kwani
suala hilo halitachukua muda mrefu na kama atakaidi basi taarifa
ataiwasilisha kwa Rais kwani ndiye mwenye dhamana ya kufuta hati miliki
ya ardhi.
Katika
mkutano huo wanachi walipata fursa ya kuuliza maswali ambapo Emmanuel
Kapalamba alimwambia wazri kuwa vijana wamekosa ardhi ya kilimo hivyo
kufanya maisha kuwa magumu kiuchumina pia kwamba hawpati huduma za umeme
na maji licha ya miundo mbinu kupita katika kijiji chao.
Kwa
upande wa wanawake walimweleza waziri kuwa kijiji hakina zahanati
kutokana na iliyokuwapo kuporwa na mwekezaji hivyo kulazimika kutembea
umbali wa kilomita 26 ili kupata huduma za afya katika hospitali ya
Chimala.
Mkutano
ulifungwa kwa waziri kuchukua baadhi ya changamoto za maji,umeme na
kilimo kuzipeleka kwa mawaziri husika ili kupata ufumbuzi wa kudumu.
Katika
ziara hiyo wazir alijionea jinsi tani zaidi ya 1800 za mpunga uliovunwa
na mwekezaji ukiwa umehifadhiwa nje ya maghala kutokana na kukosekana
na soko ndani na nje ya nchi hivyo kufanya kiwanda kuendeshwa kwa hasara
ambapo baadhi ya hecta hazijalimwa na nyingine kufanya majaribio ya zao
la soya kinyume na mkastaba.
Na Ezekia Kamanga
Mbeya yetu
0 comments:
Chapisha Maoni