BENDI ya muziki wa dansi Extra
Bongo Next Level wa zee wa Kimbembe juzi ilifanikiwa kukonga nyoyo za
mamia ya mashabiki wa muziki wa dansi waliohudhuria uzinduzi waalbamu
mpya ya bendi hiyo ya Mtenda Akitendewa uliofanyika kaika ukumbi wa DAR
LIVE MBAGALA jijini Dar es Salaam. Kivutio kikubwa katika onyesho
lilikuwa ni Mkurugenzi wa bendi hiyo Ally Choki alipoingia ukumbini na
gari la wagomnjwa Ambulance na kupanda jukwaani moja kwa moja kuanza
kulishambulia jukwaa kwa wimbo uliobeba jina la albamu Mtenda
Akitendewa.Aidha mashabiki na wadau wa muziki wa dansi walionyesa
kukunwa na ubora wa sauti za waimbaji wa bendi hiyo wakiongozwa na
Choki, Banza Stone,Athanas Muntanabe na Richard Maarifa na Adam
Bombole.Safu ya unenguaji ya bendi hiyo ikiongozwa na Super Nyamwela,
Otilia Boniface ililishambulia jukwaa kwa shoo mpya ya Kimbembe na
kuwafanya mashabiki wengi walihudhuria onyresho hilo kushindwa kutulia
vitini hali iliyoleta msisimko mkubwa ukumbini hapo.Katika onyesho hilo
Extra ilisindikizwa na bendi ya Mashujaa ambayo nayoilifanya mambo
sawasawa, huku pia malkia wa mipasho Khadija Kopa akinogesha uzinduzi
huo.
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Lina Sanga na Amin nao walikuwa sehemu
ya burudani muhimu zilizopamba ukumbini hapo na kufanya onyesho kuacha
midomo wazi wadau wa muziki waliofurika ukumbini hapo
RAIS SAMIA ASHIRIKI MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA 61 YA MAPINDUZI YA
ZANZIBAR
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
ameshiriki maadhimisho ya kilele cha Miaka 61, ya Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar y...
Siku 2 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni