Na Mwandishi Wetu
BAADA
ya kimya cha muda mrefu sasa albamu ya 'Mtenda Akitendewa' ya Extra Bongo Next
Level Wazee wa 'Kimbembe' ipo tayari kwa ajili ya mashabiki wa muziki wa dansi
kupata burudani ya kusikiliza mitupio ya sauti kama ya kundi la Wenge Musica
ambapo inatarajiwa Februari 22 mwaka huu kwenye Ukumbi wa maraha Dar Live
Mbagala jijiji Dar es Salaam.
Mtenda
Akitendewa ni albamu ya nne kwa bendi hiyo iliyoasisiwa kwa mara kwanza mwaka
2003 ikiwa na waimbaji Ally Choki, Bashiri Uhadi, Bob Kissa, Richard Maarifa,
Khalidi Chokoraa, Flora Moses, rapa Greyson Semsekwa, (solo) Bonzo Kwembe,
Efraim Joshua,George Gama (besi) Rythm na kinanda Thabit Abdul drum (ngoma)
zikipigwa na Imma Chokolate.
Albamu
ya kwanza iliitwa '3x3' ambao ni wimbo uliokuwa kwenye albamu nyimbo nyingine
ni 'Regina Zanzibar', 'Tuchunge Wazazi au Fikiri
Madinda', 'Nunu Milenium' 'Walimwengu Remix'
na 'Odise'.
Mkurugenzi
wa bendi hiyo Ally Choki alisema albamu hiyo imekamilika kwa asilimia zote na
mashabiki wataanza kuipata siku hiyo ukumbini
ambako kutakuwa na burudani ya wasanii wa
muziki wa kizazi kipya 'Bongo Fleva' wakiongozwa na Amin na Lina Sanga.
Khadija
Omar Kopa sambamba na kundi la Makirikiri wa Bongo.
Licha ya wasanii hao pia bendi ya Mashujaa
Watoto wa mama 'Sakina' itapamba uzinduzi huo huku 'Malikia wa Mipasho'.
Aidha Choki alisema, Prince Muumin Mwinjuma
'Kocha Dunia' naye ni miongoni mwanamuziki watakaoupamba usiku wa Mtenda
Akitendewa.
Extra
Bongo ilitikisa anga ya muziki wa dansi wakati huo na kuwa tishio kwa bendi
kama African Stars 'Twanga Pepeta', FM Academia, Tanzania One Theatre (TOT) na
nyinginezo hasa pale ilipoibuka na albamu ya pili iliyoitwa 'Bullet Proof'
ikiwa na nyimbo kama 'Double Double' na 'Regina Zanzibar' kabla ya kusambaratika
mwaka 2004.
0 comments:
Chapisha Maoni