Mkurugenzi wa WWF- Tanzania Bw. Bell’Aube Houinato akizungumza na waziri wa maji, Profesa Jumanne Maghembe
Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe akieleza jambo kwa wageni wake.
--
Na Rehema A. Omari
Waziri
wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe jana amekutana na Mkurugenzi mkazi wa
Mfuko wa Wanyamapori Duniani (WWF) Bell’Aube Houinato jana makao makuu ya
Wizara ya Maji, Ubungo jijini Dar es Salaam kujadili mambo mbalimbali
yanayohusu Sekta ya Maji.
Bw.
Bell’Aube alimuelezea Waziri wa Maji kwa ufupi kazi ambazo WWF
inazifanya Tanzania na namna ambavyo Sekta ya Maji inahusika katika
shughuli za utunzaji wa mazingira pamoja na viumbe hai.
Pia
alichukua fursa hiyo kumshukuru Profesa Maghembe pamoja na Serikali kwa
ushirikiano wanaotoa kwa shirika hilo. “ napenda kuishukuru Wizara yako
pamoja na serikali kwa ujumla kwa ushirikiano ambao mmelipatia shirika
la WWF” alisema Bell’Aube
Mratibu
wa Programu za Maji, Kelvin Robert ambae aliambatana na Mkurungezi
huyo, alieleza kwamba WWF -Tanzania kwa sasa ina programu tano
zinazohusu Viumbe aina, Bahari, Maji, Misitu na Mashirika ya Kiraia.
Ambapo katika programu ya maji, WWF imekua ikifanya kazi na Mabonde ya
Maji ya Rufiji, Ziwa Victoria, Wami Ruvu na bonde la Pangani ambapo kazi
yao kubwa ni kushirikiana na Ofisi za Bonde katika kuunda vyama vya
watumiaji maji, kujenga uwezo katika Usimamizi wa Rasilimali za Maji,
elimu ya mazingira na uhifadhi wa vyanzo vya maji na kuwawezesha
wananchi kufanya shughuli mbadala.
Baada
ya kupata taarifa hiyo fupi Profesa Maghembe alishauri zitafutwe mbinu
za namna gani wananchi wanafaidika na programu ya maji ya shirika hilo
“ni kitu gani mnawafanyia wananchi ili wawezekufaidika na shughuli zenu,
kama mnatunza mazingira wananchi wanafaidika vipi na utunzaji huo.
Inabidi mtafute njia ambazo mnaweza kuwasaidia wananchi kupata maji
pamoja na kwamba shughuli zenu ni za kimazingira. Alisema Waziri
Maghembe.
Profesa
Maghembe pia alisisitiza kwamba ni muhimu shirika hilo lifanye kazi kwa
karibu na Idara ya Rasilimali za Maji ili waweze kuona ni namna gani
wanaweza kufikia lengo la kuwapatia wananchi maji.
Aidha
Bw. Bell’Aube alimueleza Profesa Maghembe kwamba katika mpango kazi wao
wa miaka mitano ijayo swala la Usimamizi wa Rasilimali za maji ni moja
kati ya vitu muhimu ambavyo wanataka kuvifanyia kazi kwa karibu
wakishirikiana na wadau wengine ambao wanaweza wakasaidia katika
kusaidia katika Sekta ya Maji.
0 comments:
Chapisha Maoni