Mheshimiwa Agrey Kayombo Diwani wa kata ya vijibweni akieleza kwa undani zaidi mustakabari wa upimaji wa viwanja unaofanywa na jiji.
Mheshimiwa Baraba N.Albert Kaimu Mkuu wa Idara ya mipangomiji na Maliasili akieleza maswala juu ya mipangomiji inayoendelea katika Wilaya ya Temeke.
Mheshimiwa Sannya Bunaya Diwani wa kata ya kimbiji akitoa ufafanuzi juu ya maswara yanayohusu utoaji wa vibari vya viwanja vya kigamboni unaofanywa na Halmashauri ya jiji kinyume na utaratibu wa Halmashauri ya Wilaya ya temeke.
Mheshimiwa Mhagama Diwani wa kata kigamboni akifafanua mambo mbalimbali yanayohusu upimaji wa viwanja unaoendelea kwenye kata yake.
Hawa ni baadhi ya wajumbe katika Halmashauri ya Wilaya hii ya Temeke wakifuatilia kwa undani hoja zilizokuwa zikitolewa na Waheshimiwa Madiwani katika kikao kilichohitishwa Manispaa ya Temeke.
Watatu kutoka kushoto ni Mhandisi mkuu wa Manispaa ya Wilaya ya Temeke nd.Rickson P.Lima akiwa na wasaidizi wake wakifuatilia kwa undani zaidi masuala ya upimaji wa viwanja kigamboni hasa mji mpya.
Baraza la Madiwani wa Wilaya ya Temeke lilifanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Temeke likiongozwa na Mwenyekiti wake Mh.Mstahiki Meya Wa wilaya ya Temeke Pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo nd.Photidas Kajimba.
Lengo la Baraza hili la Madiwani ni kujadiri Miradi ya Maendeleo iliyotekelezwa na pamoja Changamoto zake na huwa linahitishwa kila baada ya Miezi Mitatu.
Kikao hicho kiliazimia Mradi wa Viwanja uliopo jiji urudi katika Manispaa ya Temeke na kutokana na wao Kama Manispaa hii ya Temeke hawanufaiki na chochote.
Mradi huu unaifanya Manispaa ya Wilaya ya Temeke kupoteza,kupata Hasara ya Sh.Bil.3 kutokana na jiji kusimamia mradi huu na kunufaika wenyewe.
Katika kikao cha jiji kinaundwa pamoja na wajumbe kutoka Manispaa hii ya Temeke ambao ni Mstahiki Meya,na Madiwani wawili.
Waheshimiwa Madiwani walisema ya kuwa Kampuni ambayo inaendesha shughuri hizi za upimaji ya KDS hawana imani nayo kwa kuwa wamevunja mahamuzi ya mikataba na Waheshimiwa Madiwani na Wabunge wametaka Viwanja vyote virudi mikononi mwa Halmashauri wawajibike wenyewe.
Jumla ya Viwanja vilivyokuwa vikiuzwa vilikuwa 2062 na mpaka sasa vimebaki 1000.
RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN ATOA POLE AJALI YA KARIAKOO
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
akitoa salamu za pole kwa waathirika wa ajali ya kudondokewa na gorofa
Kariakoo Jij...
Wiki 1 iliyopita
0 comments:
Chapisha Maoni