SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeteua kikosi cha makocha 40 kutoka sehemu
mbalimbali, Tanzania Bara na Zanzibar ili kung’amua vipaji katika mpango wa
kuboresha timu ya Taifa (Taifa Stars).
Makocha
hao ambao watafanya kazi hiyo katika michuano maalumu ya mikoa wanatakiwa kuripoti
katika ofisi za TFF siku ya Jumamosi (Februari 8 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwa
ajili ya kupewa maelekezo zaidi.
Walioteuliwa
ni Abdallah Hussein (Kilimanjaro), Abdul Mingange (Dar es Salaam), Ali Bushiri
(Zanzibar), Ali Mayay (Dar es Salaam), Ally Mtumwa (Arusha), Ayoub Selemani
(Zanzibar), Boniface Pawasa (Dar es Salaam), Dan Korosso (Mbeya), Dk. Mshindo
Msolla (Dar es Salaam) na Edward Hiza (Morogoro).
Elly
Mzozo (Dar es Salaam), Fred Minziro (Dar es Salaam), George Komba (Dodoma),
Hafidh Badru (Zanzibar), Hamimu Mawazo (Mtwara), Idd Simba (Mwanza), Jabir
Seleman (Zanzibar), John Tegete (Mwanza), Juma Mgunda (Tanga) na Kanali mstaafu
Idd Kipingu (Dar es Salaam).
Kenny
Mwaisabula (Dar es Salaam), Khalid Abeid (Dar es Salaam), Madaraka Bendera (Arusha),
Madaraka Selemani (Dar es Salaam), Mbarouk Nyenga (Pwani), Mohamed Mwameja (Dar
es Salaam), Musa Kissoki (Dar es Salaam), Nicholas Mihayo (Dar es Salaam),
Patrick Rweyemamu (Dar es Salaam) na Peter Magomba (Singida).
0 comments:
Chapisha Maoni