UCHAGUZI
Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA),
uliokuwa umepangwa kufanyika Februari 16 umesogezwa mbele kwa wiki mbili
na sasa utafanyika Machi 2, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Uamuzi
wa kusogeza mbele tarehe ya kufanyika uchaguzi huo imechukuliwa na
Sekretarieti ya TASWA kutokana na sababu mbalimbali, lakini kubwa ni
kutoa nafasi kwa wanachama wengi zaidi kulipia ada zao kwa ajili ya
kushiriki mkutano huo wa uchaguzi.
Hadi
kufikia leo mchana idadi ya wanachama waliokuwa wamelipia ada ni 57
kati ya wanachama karibu 150 waliopo katika leja na kati ya waliolipa ni
wanne tu ndiyo wamelipia ada ya miaka mitatu kama walivyotakiwa wakati
waliobaki wamelipia mwaka mmoja.
Kumekuwa
na changamoto mbalimbali zimejitokeza katika suala hili la kulipia ada,
ikiwa ni pamoja na maombi ya baadhi ya wanachama walipie mwaka mmoja na
kisha ada nyingine chama kiwawekee utaratibu wa kulipa siku za usoni
kadri itakavyoonekana inafaa.
Kutokana
na hali hiyo sekretarieti ya TASWA imepokea maombi hayo na kwa vile
uamuzi huo ulifikiwa na kikao cha Kamati ya Utendaji ya TASWA,
itayawasilisha kwenye kikao kama hicho kitakachofanyika Jumatatu
Februari 17 kujadili masuala mbalimbali yahusiyo mkutano huo, ikiwa ni
pamoja na kupitia orodha ya wanachama wanaostahili kushiriki mkutano wa
uchaguzi.
Hatua
ya awali ambayo imefanyika ni kusogeza mbele tarehe ya mwisho ya
kulipia ada, ambayo awali ilikuwa Februari 4 na sasa itakuwa Februari 15
mwaka huu saa kumi alasiri na hakutakuwa na muda wa ziada.
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
07/02/2014.
0 comments:
Chapisha Maoni