Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na wageni waalikwa
kwenye sherehe za Usiku wa Wasanii na Waandishi wa Habari zilizofanyika
usiku wa tarehe 2 Februari kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Mbeya.
Mbunge
wa Mbinga Magharibi Kapteni John Komba akizungumza na waandishi wa
habari na wasanii wa muziki na sanaa za filamu Tanzania kwenye siku ya
Usiku wa Wasanii na Waandishi wa Habari uliofanyika kwenye ukumbi wa
Halmashauri ya Mji wa Mbeya, katika usiku huo Komba alisisitiza wasanii
kuangalia maisha yao ya mbele na sio sasa kwani wasipojiandaa wataaibika
hapa ulimwenguni pia alisisitiza juu ya maslahi ya wasanii kuongezwa
kutokana na kazi kubwa wanazofanya na thamani ya kazi wayofanya.
Wasanii wakimpongeza Kapteni John Komba kwa wosia mzuri aliotoa juu yao .
Msanii
Maarufu nchini Hafsa Kizinja akitumbuiza siku ya usiku wa Wasanii na
Waandishi wa Habari,Februari 2 mjini Mbeya ,siku ambayo CCM
ilisheherekea miaka 37 ya kuzaliwa kwake na kitaifa sherehe hizo
zilifanyika mjini hapo.
Waandishi
wa habari kutoka vyombo mbali mbali wakijumuika kumshangilia Mwenyekiti
wao wa Kikosi cha Ziara mkongwe Richard Mwaikenda akijimwaga wakati wa
sherehe za Usiku wa Wasanii na Waandishi wa Habari zilizofanyika tarehe 2
Februari siku ambayo CCM ilisheherekea kutimiza miaka 37 ya kuzaliwa
kwake na sherehe kufanyika kitaifa mkoani Mbeya.
Wasanii wa tasnia ya Filamu wakiwa wamepozi kwenye sherehe za usiku wa Wasanii na Waandishi
Msanii
wa Siku Nyingi nchini Dokii akisalimiana na Mwigulu Lameck Nchemba
Naibu Waziri Wizara ya Fedha (Sera) wakati wa sherehe za usiku wa
Wasanii na waandishi wa Habari.
Baadhi
ya waandishi kutoka Jjiji la Mbeya wakipata vinywaji na maongezi kidogo
wakati wa sherehe fupi za kukutana pamoja na waandishi na wasanii wa
muziki na filamu zilizofanyika tarehe 2 Februari mjini Mbeya.
Waandishi
wa Umoja wa Waandishi wa Habari mkoani Mbeya wakizungumza na Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati wa sherehe fupi za
kupongezana kwa kazi nzuri wakati wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa
kwa CCM lakini pia usiku huo ulipewa jina la Usiku wa Wasanii na
Waandishi wa Habari.
Wasanii wakongwe wa tasnia ya filamu Tanzania nao walikuwepo kutoka kushoto ni Baba Haji, JB na Rich.
Kila mtu maarufu alikuwepo kwenye tasnia ya sanaa za maigizo na filamu.
Malkia wa Taarab nchini Hadija Kopa akitoa vionjo vya nyimbo yake mpya ambacho kinasema hata Obama anamjua.
Katibu
wa NEC Itikadi na Unenezi wa CCM Nape Nnauye akiimba sambamba na band
ya TOT wakati wa usiku uliopewa jina la usiku wa Wasanii na Waandishi wa
habari.
0 comments:
Chapisha Maoni