BONANZA LA UCHANGIAJI DAMU LAFANYIKA

Mbunge wa Afrika Mashariki na kati Mh.Angera Kiziga  pamoja na Mbunge wa Kigamboni Mh.Ndungulile katikati na Diwani wa Chang'ombe Mh.Noeli wakiwa katika maandamano ya kuashiria ufunguzi wa kongamano la Uchangiaji damu kwa hiari lililofanyika Dar Live mbagala. 




 Mh.Mbunge wa Afrika Mashariki na kati ndugu Angera Kiziga na Mh.Faustine Ndungulile Mbunge wa Kigamboni wakiwa mfano wa wachangiaji damu wakichangia damu katika viwanja vya Dar Live Mbagala.
Umati wa vijana wa wakimbiaji (jogging)wakiwa katika maandamano kuelekea katika mpango wa uchangiaji damu salama kwa hiari katika kiwanja cha Dar Live Mbagaladamu salama kwa hiari katika kiwanja cha Dar Live Mbagala.

Mh.Angera kiziga sambamba na Mh.Faustine Ndungulile wakiwa katika zawadi za pamoja walizotunzwa na umoja wa kikundi cha mazoezi (JOGGING)cha Magenge juu ambacho ndicho kilichokuwa wenyeji wa kongamano hili.


Mh.Faustine Ndungulile akiwa pamoja na wanamichezo wa kikundi cha Magenge juu katika kusakata Rumba katika ukumbi wa Dar Live.

Jumla ya watu walikuwa ni zaidi ya alfu 8 ambao walihudhuria katika kongamano hili la uchangiaji damu wa hiari lililofanyika katika ukumbi wa Dar Live mbagala.Wenyeji wa kongamano hili walikuwa Vijana toka kikundi cha Magenge juu kilichopo Mbagala mwisho.


Kikundi hiki kinajishughurisha na ufanyaji wa mazoezi kila jumapili pamoja na kuanzisha shughuli mbalimbali kama kuweka mradi wa bodaboda ambao bado haujakamilika kutokana na kuwa na kiasi kidogo cha pesa ambacho kinakadiliwa sh.mil.4 ambazo hazitoshi kwa kununua bodaboda hizo kiasi mpaka sasa wanatafuta wadhamini wajitokeze kukisaidia kikundi hicho.

Kikundi hiki cha Magenge juu ni mkusanyiko wa vijana toka sehemu mbalimbali za jiji la Dar Es Salaam waliokaa na kufikiri jinsi ya kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha kundi ambalo litakuwa kikijishughurisha na miradi mbalimbali ambayo itawawezesha kupata mikopo pamoja na kupiga hatua katika maisha.

Kongamano hili kweli lilifana kiasi ambacho Mgeni Rasmi Mbunge wa Afrika Mashariki na Kati Mh.Angera Kiziga kuwachangia Sh.taslimu Mil.1.5 akifuatiwa na Mbunge wa Kigamboni Mh.Faustine Ndungulile aliyechangia Sh.Mil 1 pamoja na Diwani wa Chang'ombe Mh.noeli ambaye aliwachangia vijana Sh.Laki 5.

Wadhamini wa kongamano hili walikuwa ni Mfuko wa Pension wa PSPF,Akiba Commercio Bank,pamoja na Bank ya Damu Tanzania ambao wote kwa kiasi kikubwa Shukrani ziende kwao kwa kuwezesha kongamano hili kwenda sawa sawia kiasi ambacho vijana wengi walijitokeza kuchangia damu.kampeni hizi zilianzishwa na mbunge wa Kigamboni Mh.Faustine Ndungulile ambaye kwa kiasi kikubwa anawahamasisha vijana katika mambo ambayo yanaweza kuwaletea maendeleo wayafanye kwa kuzingatia katiba ya nchi yetu ya Tanzania.

Mh.Ndungulile aliiomba Serikali kuangalia vikundi vya vijana ambavyo vinajikusanya katika kutafuta miradi mbalimbali ili ijikwamue kimaisha waweze kupata fedha kwa liba nafuu katika mabenk na saccos zilizopo Tanzania.Vijana wengi waige mfano wa kikundi hiki cha magenge juu wanachokifanya kwani ni mfano tosha wa kuigwa hapa nchini kwetu. 




Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List